Pages

Mawaziri wa fedha wa nchi za ukanda wa afrika wajadili maendeleo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali wa

Dkt. Servacius Likwelile akiwa pamoja na Kamishina wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya wakati mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Abidjan.

Akizungumza na vyombo vya habari mchana huu DKt.Likwelile ambaye ni amemuwakilisha Waziri wa Fedha na katika Mkutano wa Benki ya Dunia amesema kuwa,”Mkurungezi wa Kanda ametoa ripoti ya mwaka,  ameelezea ni namna gani ukanda huu wa Afrika ulivyokuwa ukifanya kazi za maendeleo, ameelezea ripoti hiyo kuwa inagusa nchi zote sita za Afrika. Nchi hizo ni pamoja na Rwanda, Tanzania,Uganda, Kenya, Ethiophia na Visiwa vya Shelisheli, Aidha nchi hizo zimefanya kazi vizuri.

Alisisitiza Likwelile. 
Likwelile amefanafua kuwa, “Mkurugenzi wa ukanda wanchi za Afrika  ameelezea jinsi uchumi unavyokua kwa kasi kubwa kwani umekua kwa  asilimia sita mpaka saba na ukuaji huu wa uchumi unawanufaisha watu  wote wa nchi hizo.

Ni Muhimu kuwekeza kwenye reli hii itawapunguzia wananchi usumbufu wanaoupata kwenye masuala ya usafiri na usafirishaji wa mizigo.Aliongeza  Likwelile.

Pia Likwelile amezungumzia kuhusu kuendeleza kilimo hasa kilimo chenye tija. alisema kuwa kilimo cha biashara humuongezea kipato mwananchi  wa chini na kumfanya kujikwamua kwenye hali ya kimasikini.

Aidha mwenyikiti amezungumzia suala nishati hasa nishati ya umeme ili  tuweze kuendelea ni muhimu kusimamia suala la umeme kwa kikanda. Hii itapelekea nchi zote za Afrika kunufaika na masuala ya maendeleo kiujumla kwa nchi hizo za kikanda.

“ Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa rais, Aidha ukanda wa nchi  za Afrika unapenda kumshukuru raisi aliyepita Dkt. Kaberuka kwa kazi  nzuri aliyoifanya kwani ameziacha nchi katika hali nzuri sana” Alisisitiza Likwelile.Mwisho Likwelile alifafanua kuwa, “Benki ya Maendeleo ya Afrika  imetambua umuhimu wa kazi na mchango mkubwa alioutoa Mhe. Jakaya  Mrisho Kikwete na ndio maana imemualika katika Mkutano huu wa mwaka  kutokana na kazi zuri aliyoifanya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)