Pages

Mangula na Nape wahani msiba wa John Nyerere

 Picha ya Marehemu John Nyerere aliyefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.

Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini  Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa Kapteni wa Jeshi la Wananchi  Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni  kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na  kisukari kwa muda mrefu.

Enzi za uhai wake John alishiriki vita ya kumng'oa Nduli Idd Amini nchini Uganda. Mungu ailaze roho ya marehemu John mahali pema peponi. AMENI
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akisaini kitabu cha rambi rambi nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam ambapo alifika kumpa pole Mama Maria Nyerere na familia yake kufuatia msiba wa mtoto wa Baba wa Taifa John Nyerere.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokutana nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam kuhani msiba wa John Nyerere.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa John Nyerere.
 Ndugu akitoa pole kwa Mama Maria Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa mkono wa pole Mama Maria Nyerere kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere kilichotokea jana jijini Dar es salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mama Maria Nyerere  alipofika nyumbani kwake kumpa pole kufuatia msiba wa mtoto wake John  Nyerere, wengine pichani ni Makongoro Nyerere (kushoto), Mwenezi wa CCM  mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi, na Anna Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Makongoro Nyerere Msasani nyumbani kwa Baba wa Taifa wakati wa kuhani msiba wa John Nyerere. (Picha zote na Adam Mzee)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)