Pages

Maandalizi ya uzinduzi wa Manjano foundation yakamilika

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser Katikati  akiongea na Vyombo vya Habari leo wakati akelezea Mandalizi ya Uzinduzi wa Manjano Foundation Ambao ni Mpango unaolenga kuwawezesha Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wasichana wa Kitanzania.Mpango Uzinduzi
huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Utatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi..Mgeni Rasmi anategemewa Kuwa Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda

 Meneja Mradi wa Manjano Foundation Mama Gugu Ndolvu Akieleza jambo leo wakati wakiongea na wanahabari kuhusu Mradi huo ambao ni Mkombozi kwa wakinamama wasio na Ajira Akiwa samabamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  Pamoja na  Aunty Sadaka Gandi
 Aunty Sadaka Gandi akiwa ni dada mkuu wa Atakayewashauri wasichana watakaopata mafunzo ya ujasiriamali kupitia Manjano Foundation. 
Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango hup wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  

Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwani Balozi Mwanaidi Majaar. Shear Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania kwa Zaidi ya miaka kumi. Wamebaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele, vipodozi na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya LuvTouch Manjano.


LuvTouch Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza muonekano wako kwa hali yoyote.
Shear Illusions inazishukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI, Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)