Pages

Lowasa aanza safari ya matumaini leo

Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa likipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehemu ya kutangaza nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)