Pages

Kipindupindu tishio katika kambi ya wakimbizi wa burundi nyarugusi, Oxfam yatoa msaada

 Baadhi ya wakimbizi wakiwa wamewasili Kigoma
 Wakimbizi kutoka Burundi wakisubiri huduma mbalimbali za kijamii
 Mmoja wa wakimbizi akiwa anapata matibabu
 Hapa watoto wa wakimbizi wakijipikia Chakula , katika mazingira hatarishi
 Mamia ya wakimbizi wakiwa wanatafakari hatima yao
 Hii ndio hali halisi ya vyoo ambavyo vimechangia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
Wafanyakazi wa Shirika la Oxfam wakishusha vifaa kwa ajili ya vifaa vya upatikanaji wa maji na vyoo ili kubabiliana na Kipindupindu. 
 Hiki ni moja ya chanzo cha maji
 Wakimbizi wakiwa ndani ya Meli


Ongezeko la wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi pamoja na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo maji safi linamaanisha
kuongezeka kwa hatari ya mlipuko wa magonjwa ya kuambukizwa hasa kwa
wakimbizi takribani 40,000 walioko Kagunga mpakani mwa Tanzania. 

Tayari
watu 20 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo
ya Kagunga na katika kambi ya Nyarugusu ambapo wakimbizi hupelekwa kwa
ajili ya makazi.

Shirika
la Umoja wa Mataifa (UN) limeripoti uwepo wa watu 1057 wenye dalili za
kuharisha waliopo Kagunga ambapo wakimbizi husubiria usafiri wa boti
zinazowasafirisha kwenda Kigoma. 

Kuna
uhitaji wa haraka sana wa huduma za msingi ikiwemo maji safi na vyoo.
Shirika la Oxfam linafanya kazi na shirika la TWESA ili kutoa ufumbuzi
wa haraka kukidhi mahitaji hayo kwani kuna uhitaji wa haraka sana wa
maji safi, huduma za matibabu pamoja na vyoo. 

Shirika
la Oxfam tayari limeanza maandalizi ya haraka ili kuongeza upatikanaji
wa maji safi na kujenga vyoo vya dharura katika kambi ya Nyarugusu ili
kukabiliana na ongezeko kubwa la wakimbizi. 

Inakadiriwa
takribani wakimbizi 22,000 wamesafirishwa kutoka Kagunga kwenda katika
kambi ya Nyarugusu ambapo wanapewa makazi ya muda mfupi katika shule na
makanisa wakati mashirika mbalimbali ya misaada yakiendelea kutoa vifaa
vya ujenzi wa makazi ya muda mrefu. 

Huduma za matibabu katika makambi ya wakimbizi zinasua sua kutokana na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa mbalimbali.

Uhitaji wa haraka wa huduma za msingi ni muhimu ili kuzuia ongezeko la magonjwa yanayosambaa kama kipindupindu. 




No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)