Pages

Kipindi cha Mboni show chaazimisha miaka mitatu kwa kutoa misaada

 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akimkabidhi Mkuu wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Akina mama wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dokta Mathew Kallaga (aliyepokea kwa niaba ya uongozi) vifaa mbali mbali vyenye thamani ya Tshs. Milioni saba alivyotoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitatu ya kipindi hicho. Kila mwaka Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akipongezwa meneja wa Jengo la Wazazi, Sister Amina Mwakuluzo kwa moyo aliyouonyesha. Kila mwaka Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. (Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.)
 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitoa shukrani zake kwa uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuweza kumpokea na kukubali vifaa alivyotoa ili viweze kuendelea kusaidia jamii. Mboni alitoa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya Tshs. Milioni saba alivyotoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitatu ya kipindi hicho. Kila mwaka Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akimkabidhi kikombe Mkuu wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Akina mama wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dokta Mathew Kallaga.
 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitoa zawadi mbali mbali kwa akinamama aliyowakuta katika wodi ya wazazi. Kipindi cha Mboni huwa kinaadhimisha kwa kutoa msaada sehemu mbali mbali ikiwa ni mpango wake wa kurudisha fadhira kwa jamii ambapo mwaka huu aliungwa mkono na PSPF, Nakiete Pharmacy, Fadhaget Sanitarium Clinic pamoja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akimkabidhi nguo kwa mama aliyejifungua mtoto wa kike. Pembeni anayeshikilia nguo ni Mkurugenzi wa Fadhaget Sanitarium Clinic, Dokta Fadhili Emily.

... Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akiwa amebeba mtoto kwa furaha.

 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitoa zawadi ya Nakiete Baby Diaper ambazo hutengenezwa na Kuuzwa na Nakiete Pharmacy ambao nao waliungana nae kutoa msaada huo.

 Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (katikati) akiongea machache mara baada ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya Tshs. Milioni saba alivyotoa kwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitatu ya kipindi hicho. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Fadhaget Sanitarium Clinic, Dokta Fadhili Emily, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Nakiete Pharmacy, Dorine Mzava na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Uzazi na Magonjwa ya Akina mama wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dokta Mathew Kallaga na Dokta Vicent Tarimo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea wakati alipounga mkono Kipindi cha Mboni Show katika utoaji wa Misaada katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Nakiete Pharmacy, Dorine Mzava na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akitia shukrani kwa wauguzi wa hospitali hiyo.
Picha ya Pamoja...
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutoa msaada katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba akishow ndugu zake na Emma Kahere na Mariam Masimba.
Timu ya Mboni Show ikifurahia pamoja madokta.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)