Pages

Kampuni ya ALAF yazindua Nembo mpya

 
Ni furaha yangu kubwa kuwaalika leo hii kwenye uzinduzi wa NEMBO mpya ya kampuni ya ALAF.

Nichukukue nafasi hii kuwaeleza kwa kifupi kuhusu ALAF

Kamuni ya ALAF, ilikuwa ikijulikana kama ‘Aluminium Africa Limited’, ilimetimiza miaka 50 mwaka 2011. Mwaka 1960, ALAF ilianza shughuli zake mjini Dar-es-Salaam. Kwa siku zile, ilikuwa ni kampuni ya kwanza Afrika Mashariki kuweka kiwanda cha kuzalisha chuma cha kukunjwa (kwa ajili ya masufuria), Mabati na Vyuma vigumu vya kuezekea

ALAF ilitaifishwa mwaka 1973 na kubinafsishwa mwaka 1997 na imekuwa moja kati ya stori za mafanikio katika Sera ya Serikali ya ubinafsishaji wa viwanda.

Leo hii ALAF tuna mashine za kisasa  zijulikanazo kama Cold Rolling Mill Complex zenye uwezo wa kuzalisha bidhaa kama CRC na CRCA maarufu kama ‘Metal Coating Line’ ambazo hutumika kuzalisha vyuma vya aluminium na Zinc, Mabati ya kuezekea na pia tuna mashine nyingine ijulikanayo kama Tube Mills kwa ajili ya kutengenezea mabomba ya chuma, na bidhaa nyingine mbalimbali. Teknolojia yetu ya ‘Metal Coating Line’ ni ya aina yake Afrika nzima na ilichukuliwa kutoka BIEC, Marekani.

ALAF inatoa bidhaa za kuezekea kwa ajili ya majengo ya aina zote, Mabomba ya chuma, vifaa vya aina zote vyenye nafasi kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika sekta ya ujenzi. Bidhaa za ALAF zinaaminika zaidi na ni bidhaa zinazouzika zaidi Tanzania na nchi za jirani.

Kwa bidhaa za viwandani za kudumu, ALAF inatoa SAFLOK 700, bidhaa inayosaidia kuunganishia mabati ya kuezekea mpaka mita 150 kwa urefu wakati wa kuezeka bila kutumia misumari au bolti. Baadhi ya majengo yaliyotumia bidhaa hiyo ni jengo la Mlimani City lililopo mjini Dar es Salaam, jengo la AICC Arusha, jengo la Ofisi ya waziri mkuu Dodoma na majengo mengine mengi.  

Bidhaa za ALAF zinauzwa kwenye mataifa yote ya jirani kama Zambia, Malawi, Burundi, Rwanda, Uganda n.k. hivyo basi kuingiza fedha za kigeni nchini.

Kwa miaka mingi ALAF imeendelea kugundua njia mpya na namna ya kuhudumia wateja wake vizuri kwa kutoa huduma na bidhaa zenye viwango vya kimatifa . Moja ya hatua zilizochukuliwa na ALAF ni kuwafikia wateja wake kwa Karibu zaidi. Kuhudumia wateja wake kwa ufanisi zaidi ALAF ilifungua kituo cha huduma mjini Arusha 2009, Mwanza 2012 na Mbeya 2013 kwa wateja wa mkoa wa Kilimanjaro, Kanda ya ziwa na Nyanda za juu kusini Vilevile. Kwa kuongezea, ALAF walifungua ‘Showroom’ mbili (Roof Gallery) Dar es Salaam na Arusha. Vituo vya huduma za ALAF na ‘Showroom’ zinasimamiwa na wafanyakazi wenye uzoefu na waliopewa Mafunzo ya kutosha, wanaowashauri wateja kuhusu suluhisho bora la kuezekea. Mwaka huu ALAF imepanga kifungua kituo kingine cha huduma Dodoma.

ALAF ni ya kwanza na kampuni pekee ya aina yake nchini Tanzania kupewa ISO 9001:2000 na ISO 14001:2005 kwa kuzingatia viwango vya ubora wa bidhaa zake na kujitoa kwake katika kulinda mazingira.

ALAF imekuwa ikishinda Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora wa Mwaka (kwa kundi la viwanda vikubwa) Inayoratibiwa na shirikisho la viwanda Tanzania (CTI). Kwa miaka nane ya mafanikio.

Kujitoa kwa ALAF ni zaidi ya ubora wa bidhaa zake. Kama sehemu ya kujitoa kwake kwa mazingira, ALAF imeanzisha mfumo ujulikanao kama ‘Light Weight Steel Truss System’ kuchukua nafasi ya matumizi ya mbao kutengeneza kenchi za kuezekea. Bidhaa hii inaokoa miti mingi, hivyo kuifanya bidhaa rafiki zaidi kwa mazingira.

Mabibi na Mabwana

ALAF inaendeleza jitihada za kurejesha inachokipata kwa jamii na kutimiza wajibu wake kwa jamii zaidi ya maneno. Kwa kushirikia na shirika la fedha (IFC), USA, , ALAF imezindua mpango wa elimu ya afya kwa ajili ya kuzuia na kutibu Malaria, VVU/UKIMWI na kifua kikuu si tu kwa wafanyakazi wake lakini pia kwa jamii inayozunguka viwanda vyake. ALAF ina zahanati ya kisasa yenye vifaa kamili na  mazingira bora kutoa tiba bure kwa wafanyakazi wake na familia zao. Zahanati hii inasimamiwa na madaktari, manesi na wafanyakazi wa Hindu Mandal Hospital.

Kama mwanachama muwajibikaji kwa Jamii ya raia wa Kitanzania, ALAF imetanua msaada wake kwa Mpango wa Chakula Duniani kwa watoto na kutoa mchango mkubwa kwa njia ya vifaa vya kuezekea moja kwa moja kwa miradi ya shughuli za kijamii.

Mabibi na Mabwana

NEMBO mpya ya ALAF inahusisha kiini cha kufikia ngazi mpya ya ubora ambao unaiweka ALAF nchini Tanzania na nchi jirani kama watengenezaji wakubwa na wakuaminiwa zaidi wa mabati ya kuezekea, mabomba ya chuma na bidhaa nyingine mbalimbali za ujenzi kwa viwango vya kimataifa.

Utambulisho wa NEMBO mpya ni pamoja muonekano mpya wa ALAF na ushirikiano wake na SAFAL Group ambayo ipo katika nchi 11 kuanzia Ethiopia hadi Afrika Kusini katika maeneo 33.

Kwa hili ALAF inaanza safari mpya pamoja na muonekano mpya ulioboreshwa. Jina,  Lengo na maadili ya kampuni yetu havitabadilishwa.

Tunaposonga mbele, ni muhimu kutazama nyuma kule tulipotoka na jinsi tulivyoendelea. Muonekano  wetu  mpya unatupa fursa kubwa ya kuwa na nguvu mpya.

Tunaamini kuwa washiriki wetu kibiashara watayapokea mabadiliko haya mazuri na kuendelea kutoa ushirikiano wao kwa mafanikio ya baadae.

Mabibi na Mabwana

Asanteni tena kwa kuchukua muda wenu katika ratiba zenu zenye majukumu mengi na kutoa ushirikiano kwa ALAF katika tukio hili  muhimu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)