Pages

IS wauteka mji wa Ramadi

Wapiganaji wa Islamic State
Baada ya mapigano makali kwa siku kadhaa katika mji wa Ramadi nchini Iraq,hatimaye mji huo kwa sasa unashikiliwa na wapiganaji wa kundi la IS.
Makundi ya wanajeshi wa serikali wamekimbia kutoka katika eneo hilo na Islamic State wamejitangazia ushindi dhidi ya mji huo na kwamba wanaushikilia.
Mapema msemaji wa Gavana wa jimbo hilo amesema kuwa wapiganaji hao wanayashikilia baadhi ya majengo mhimu ya serikali katika jimbo hilo.
Hata hivyo umoja wa Mataifa umelaani hatua hiyo ya IS,ambapo pia Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amesema kuwa kwa sasa wanajipanga kwa kushirikiana na majeshi ya Shia ili kukabiliana na wapiganaji hao.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)