Pages

Bodi ya UTT yaendelea na ziara ya siku tano nchini china

3.jpg pichaBodi ya taasisi ya UTT-PID na Menejimenti yake wakia katika picha ya pamoja na uongozi wa kampuni ya Chengdu Engineering Corporation wakati wa picha ya pamoja. Waliosimama mbele (wa pili kutoka kulia) ni mjumbe wa bodi Bi. Janeth Mmari, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Mrs Elpina Mlaki. Wengine ni wajumbe wa bodi hiyo ya UTT-PID pamoja na wenyeji wao wa nchini humo

Na Mwandishi Maalum
Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake iliyozuru nchini China katika ziara maalum ya siku tano kwa ajili ya Mafunzo na kubadilishana uzoefu imefana na tayari bodi hiyo imerejea nchini.

Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. Elipina Mlaki pamoja na Menejimenti nzima walieleza kuwa imeweza kuwa ya mafanikio makubwa huku wakiahidi kuyafanyia kazi yae yote waliojifunza nchini China.

Katika ziara hiyo, bodi na menejimenti ya UTT-PID walipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ya miji ya nchi hiyo ikiwemo makampuni makubwa na kujifunza na kujenga na kudumisha ushirikiano wa utendaji wa kazi.
2.jpg
Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Mrs. Elpina Mlaki (wa pili kulia) akilezea jambo katika moja ya mkutano wao waliofanya katika ziara hiyo nchini China. Anayemfuatia ni Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha pamoja na wajumbe wa bodi na Menejimenti ya UTT-PID, Wengine kushoto ni watendaji kutoka kampuni ya Chengdu Engineering Corperation ya nchini humo.

UTT-PID Mafanikio yake nchini

DAR ES SALAAM-Moja ya mafanikio ya Taasisi ya UTT-PID ni pamoja na uwekezaji na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa na ghorofa 20 mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam kwa matumizi mbali mbali ya kiofisi na biashara.

UTT-PID kwa kushirikiana na muungano wa Vyama vya Ushirika Tanzania walifanikisha ujenzi wa jengo hilo lililopewa jina la ‘’Ushirika Building’’ na kufunguliwa mwaka 2013 na Mhe Rais Jakaya M. Kikwete. Mradi huu pia unajumuisha pia ukarabati wa jengo la zamani ambao unaendela kwa kasi nzuri.

LINDI-Mafanikio mengine ya Taasisi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya upimaji wa ardhi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanja 10,000 katika mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ambapo awamu ya kwanza viwanja 2,473 vilipimwa katika Pwani za Mabano na Mmongo na hadi sasa Taasisi kwa kushirikia na Halmashauri ya Lindi wanaendeleza kazi ya uuandaji wa hati kwa ajili ya wanunuzi ikijumishwa na upanuzi wa barabara katika eneo la mradi.
IMG_6955.jpg piha
UTT-PID wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao katika baadhi ya miji ya nchini China walipotembelea kwa ziara ya mafunzo ya siku tano ya kujenga uzoefu na ufanisi wa utendaji wa kazi za Taasisi hiyo.
KAGERA-Katika mkoa wa Kagera, Taasisi kwa ushirikiano na Halmashauri ya Bukoba iliwezesha na kusimamia upimaji wa viwanja 5,000 vya matumizi mbalimbali ambapo hadi sasa viwanja 3500 vimeshagawia kwa waombaji mbalimbali.
Uwekezaji huu umeigharimu Taasisi hii zaidi ya fedha za kitanzania kiasi cha Billioni kumi ( Bilion 10) katika uendeshaji miradi mbalimbali na uwekezaji wa miundombinu kama vile maji, umeme na uchongaji wa barabara.
MIKOA MINGINE- Miradi mengine mikubwa iliyofanywa na Taasisi inajumuisha pamoja na wa Mapinga Bagamoyo ambapo uwekezaji wa miundombinu husika kama maji, umeme na barabara umekwisha fanyika, sehemu nyingine ni pamoja na Kingolowira na Kiegea Morogoro, Soga Kibaha na Sengerema Mwanza.
IMG_6985.jpgyyy
Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Mrs. Elpina Mlaki (mwenye skafu nyekundu) wakisikiliza maelezo kwa umakini kutoka kwa wataalamu wa kampuni ya Chengdu Engineering Corporation walipotembelea katika nchi ya China kwa ziara ya mafunzo ya siku tano. (kulia kwake) ni mjumbe wa bodi hiyo, Mrs. Janeth Mmari.
IMG_6971.jpg uuuMwanasheria wa UTT-PID, Bi Tuzo Mpiluka (kushoto) akiwa pamoja na Afisa Majengo mwandamizi wa UTT-PID, Ndugu Sebastiaan Ivambi (katikati) wakiwa pamoja na mwenyeji wao Mr. Donny Yang wa Power China, katika ziara hiyo ya siku tano, nchini China ya jujenga uzoefu.
IMG-20141003-WA0000.jpgww
Moja ya miradi ya UTT-PID uliopo Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani, Tanzania, ambapo uwekezaji wa miundombinu husika kama maji, umeme na barabara umekwisha fanyika, kama unavyoonekana pichani katika sehemu ya mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)