Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke wakiwa katika hatua ya mwisho ya kujumuisha alama za washiriki kwaajili ya kuwataja washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi na tano bora.
Baadhi ya washiriki wakiwa mbele ya meza ya majaji (hawapo pichani) kwaajili ya kutajwa kama wamefanikiwa kuingia katika hatua ya 15 ambapo mara baada ya hatua hiyo washindi watatu kutoka kanda ya ziwa mkoani Mwanza waliweza kupatikana na kukabidhiwa kitita chao.
Mmoja wa washiriki akiwa anamshukuru Muumba wake mara baada ya kutangazwa kufanikiwa kuingia katika washiriki 15 bora.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 #mpakakieleweke limeingia hatua ya tatu na ya mwisho ambayo imepelekea kuwapata washindi wa tatu wa kwanza kutoka kanda ya Ziwa Mkoa wa Mwanza.
Shindano hili limechukua sura mpya mara baada ya vijana wengi kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kushiriki shindano na hatimaye limeweza kufanyika kwa ustadi na mafanikio makubwa. TMT 2015 #mpakakieleweke kwa mwaka 2015 limeanzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza na huku washindi watatu wakipatikana na kukabidhiwa zawadi zao za Shilingi Laki tano Kila Mmoja huku wakisubiria kuelekea jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki kwenye kinyanganyiro cha kuwania Zawadi kubwa kabisa kwa mshindi mmoja wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke ya shilingi za Kitanzania Milioni 50.
Mara baada ya kumalizika kwa Shindano hili la TMT 2015 #mpakakieleweke kwa kanda ya ziwa Mkoani Mwanza, shindano hili litahamia Kanda ya Kaskazini Mkoa wa Arusha ambapo usajili utafanyika tarehe 1 na 2 Mwezi wa 5 katika ukumbi wa Triple A, uliopo Jijini Arusha.
Shindano hili la TMT 2015 #mpakakieleweke limekuwa shindano lenye mvuto mkubwa katika Jamii ya kitanzania kutokana na kufanya vizuri kwa awamu ya kwanza na kupelekea Vijana wengi kuonyesha vipaji vyao.
Kipindi cha kwanza cha Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke kitarushwa hewani na kituo cha Runinga cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku.
TMT 2015 #mpakakieleweke imepigwa tafu na Precision Air, Global Publishers, I-View Studio pamoja na ITV/Radio huku makampuni mengine yakikaribishwa katika kushirikiana na kampuni ya Proin Promotions ambao ndio waendeshaji wa shindano la TMT (Tanzania Movie Talents) .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)