Pages

Tanzania kupambana na Ukosefu wa Lishe bora

 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akisalimiana na mwakilishi kutoka UNICEF katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akisikiliza kwa makini hoja iliyokuwa ikitolewa na mwakilishi kutoka CIFF katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC.
 Wajumbe kutoka nchi mbali mbali Duniani wakimsikiliza Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya ( hayupo kwenye picha) alipokuwa akiwasilisha mada na kuchangia hoja mbalimbali katika mkutano uliohusu Lishe bora kwa mtoto mjini Washington DC.
 Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akitoa mada na kuchangia hoja mbalimbali zinazohusu Tanzania katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC. 
Lishe bora ni msingi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano ambao ulikuwa unazungumzia kuhusu
suala la Lishe (Nutrition).

"It is
important to understand consequences including adverse effects on the child's
physical and mental development from conception until it reaches the age of
two. These effects are irreversible," he said.
"Ni muhimu kuelewa madhara yatakayompata mtoto ikiwa mama hata mnyonyesha mtoto huyo ikiwa ni pamoja na athari mbaya juu ya mwili na maendeleo ya mtoto kutoka mimba mpaka kufikia umri wa miaka miwili  kama mtoto hatapata Madhara haya ni kubatilishwa.," Alisema  Mkuya.
Mkuya aliongeza kuwa, “ Tanzania tunajitahidi sana kupambana na janga hili kwani mama kushindwa kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita kunaweza kusababisha utapiamlo na kusababisha kuathiri mamilioni ya watu katika Tanzania, hasa watoto, na hivyo kusababisha magonjwa kuenea na kunyong’onyesha maendeleo ya kimwili na ki akili”.

“Kwa kuruhusu hali hiyo kunachangia kupunguza uwezo katika kuboresha uwezo wakufikiri, kupunguza nguvu ya  kujifunza na kuwa mbunifu, kuongezeka kwa umaskini, na kasi ndogo katika kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi”.Aliongeza Mkuya.

Takwimu za mwisho za utafiti wa mambo ya afya zina onyesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 5-59 wana upungufu wa madini,asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa vitamin A.  Asilimia 11 ya wanawake wenye umri wa kuzaa yaani  miaka 15-49 wana uzito wa chini, asilimia 41 wana uzito wa chini na upungufu wa madini, wakati asilimia 58 ya mama wajawazito wana upungufu wa
madini pia.

“Katika Tanzania mikoa ambayo inafanya vizuri katika kupambana na utapiamlo ni mkoa wa Kilimanjaro, Mjini magharibi na Mkoa wa Dar es salaam.”  Alisema Mshauri  Lishe wa Rais Jakaya Kikwete”.Dr. Wilbald
Lori.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na janga hili, hivyo katika mikutano hii mikakati mbalimbali inapangwa ya jinsi ya kulimaliza kabisa tatizo hili. Mikutano hii bado inaendelea na hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi. 

Imetolewa na
Msemaji :Wizara ya fedha
 Ingiahedi C.Mduma
Washington DC

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)