Pages

Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke yaingia hatua ya pili Kanda ya Ziwa

 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) season 2 #mpakakieleweke wakiwafurahi mara baada ya kufurahishwa na mmoja wa washiriki walioingia kwenye usaili wa shindano hilo linaloendelea kufanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ambao usaili umeingia hatua ya pili ya washiriki kupewa mwongozo (script) kwaajili ya kuelekea fainali
 Mshiriki akionyesha kipaji chake mbele za majaji (hawapo pichani)
 Haya huyu nae na kisu ila ndo hivyo yote ni kuonyesha vipaji tu
 Wakisoma script waliyopatiwa kwaajili ya kuingia hatua ya pili ya usaili katika shindao la TMT 2015 #mpakakieleweke
Wakiifanyia mazoezi script kwaajili ya hatua ya pili ya Usaili wa shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke, TMT 2015 #mpakakieleweke imepewa sapoti na Presicion Air, Global Publishers, I-View pamoja na ITV na Radio One.

Pamoja na usaili huu kuendelea kufanyika kutakuwa na Uzinduzi wa filamu ya Washiriki wa TMT 2014 ambapo itaonyeshwa kwa mara ya kwanza leo katika Ukumbi wa Isamilo Jijini Dar kwa kiingilio cha Elfu Tatu kwa washiriki wa TMT mwaka huu huku wengine wakilipa elfu tano tu.

Vilevile Filamu hii itazinduliwa katika mikoa yote tutakayopita ya TMT.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)