Pages

Polisi watumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu Iringa mjini

Askari  wa FFU wakiwa katika msako  wa  kuwasaka  waliohusika na  vurugu hizo eneo la Ipogolo  mjini Iringa
Moshi wa  bomu la machozi  ukiwa angani
Askari  wa zimamoto  wakizima moto katikati ya  barabara  ya  Iringa - Kilolo  leo
Askari  wa zimamoto  wakifungua  barabara
Askari  wa FFU  wakiwa kazini
Askari  wa Zimamoto akitoa  taili  lililokuwa  likiwaka barabarani
Wananchi  waliokuwa  msibani  wakishuhudia msako  mkali wa  polisi
Barabara  ikiwa  imefungwa
Askari  wa jeshi la  Zimamoto na  uokoaji mjini Iringa  akisaidia kumvusha  mzee  ambae  alikuwa akikimbia mabomu na  kujificha mtaroni
Mzee  huyo  akimpongeza  askari kwa  wema  wake
Baadhi ya  watuhumiwa wa  vurugu hizo  wakipakiwa katika gari la  FFU 
Wananchi  wakiwa katika  vurugu  hizo  huku baadhi yao  wakishuhudia

Mpita njia  eneo la Ipogolo akipiga  picha kwa simu moto  uliokuwa  ukiwaka barabarani

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU mchana huu wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wameziba barabara ya Iringa -Kilolo kwa kuchoma mataili


Wananchi hao wamefikia uamuzi huo Baada ya mtoto kugongwa na gari kwa zaidi ya saa Moja bila maiti kutolewa.

Kutokana na hali hiyo wananchi hao wa Eneo la Ipogolo walilazimika kuchoma moto barabara hiyo huku waliochoma mataili Kabla ya Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya

 Na  MatukiodaimaBLOG


VURUGU  
kubwa  zimetokea leo   katika  eneo la Ipogolo  mjini Iringa na  
kupelekea askari wa   kikosi cha kutuliza  ghasia  (FFU)  kutumia   
mabomu ya 
machozi  kuthibiti vurugu    baada ya mtoto wa  miaka kata 6 
kugongwa na gari  wakati  akifanya biashara ya  kuuza mbogo mboga .

Wananchi wanaosadikika  kuwa na  hasira kali  walianza kuwashambulia
askari  polisi waliofika kuchukua mwili huo kwa mawe  kwa madai ya   
kuchelewa  kufika  eneo la  tukio.


Wakizungumzia  
tukio   hilo kwa mwandishi wa habari hizi  baadhi ya  wananchi
walisema  kuwa  mtoto   huyo  aligongwa  majira ya saa 7 mchana na zaidi 
ya saa  moja baada ya  kutoa taarifa  polisi  ndipo  walipofika  eneo 
la  tukio jambo lililowakwaza  wananchi hao .

Walisema  kuwa  mbali ya  polisi  hao  kufika  pia tayari  baadhi ya askari    waliopo eneo hilo la stendi kuu ya Ipogolo  kwa  kushirikiana na   wananchi  walifanikiwa  kulikamata  gari  ambalo  lilisababisha ajali   hiyo .

Alisema   Neema Sanga  kuwa wakati  tukio  la kugongwa  mtoto  huyo  likitokea   
alikuwa jirani na eneo hilo katika  msiba  na kuwa  wakati  akiwa  
ameingia ndani ya nyumba  hiyo  yenye msiba  kusaidia  kugawa  chakula 
ghafla  alipata taarifa  kuwa wananchi  wameanza vurugu kwa  kuchoma   
moto mataili katika barabara  hiyo  kuu ya  Iringa- Kilolo.


Hata   
hivyo  alisema  kuwa  tukio  hilo  lilichukua  zaidi ya dakika 45   
polisi  hao wa FFU  kufika na kuanza  kutuliza  vurugu  hizo kwa  kupiga 
mabomu ya  machozi  kuwatawanya  wananchi zaidi ya 500  waliokuwa   
wamekusanyika eneo hilo kuzuia  magari  kuendelea kupita katika  
barabara  hiyo  huku  baadhi yao  wakitaka  kufunga  barabara  kuu ya  
Mbeya  - Iringa ambayo haihusiki ka bisa na   eneo  lililotokea  tukio 
hilo.


"
Ni  kweli  mtoto kagongwa na gari na kufa  tukio ambalo ni kusikitisha 
sana na  polisi baada ya  kupigiwa simu  wamefika  eneo la  tukio na  
kuchukua maiti ya  mtoto  huyo lakini  tunajiuliza kwanini  vijana hao 
kuanza  kuwapiga mawe  polisi na kufanya  vurugu  wakati gari  
lililogonga mtoto huyo  likiwa  limekamatwa .."  alihoji Bi  sanga


 Kuwa 
kwa  upande  wake hakuona  sababu za  polisi  kupigwa  wala  wananchi  
hao kuchoma moto  barabara wakati ajali  hiyo kama ajali nyingine na  
tayari  gari  lililosababisha ajali  likiwa  limekamatwa .


Bi  
Sanga  alisema  wakati  mwingine  polisi  wanalalamikiwa kuwa 
wanatumia  nguvu  zaidi  ila kwa  tukio   hilo lawama  zake anazipeleka 
kwa  wananchi wenzake ambao walionyesha  kufanya vurugu kwa kuchomo 
moto  barabara  hiyo ya lami na   kupiga  polisi huku  wakitambua  wazi 
polisi si  waliosababisha ajali  hiyo.


 Huku 
kwa  upande  wake mmoja  John Kalinga  akiomba  serikali kupitia  
wizara ya miundo  mbinu  kuangalia   uwezekano  wa  kuweka matuta katika
eneo hilo kwa madai kuwa  hii ni ajali ya  pili  kutokea na  
kusababisha  vifo  toka  eneo hilo  lilipowekwa  lami .


Mwandishi  
wa habari hizi  alishuhudia baadhi ya  vijana  wakikimbilia kujificha  
katika nyumba  moja  iliyopo eneo hilo ambayo  ilikuwa na msiba   huku  
baadhi yao  wakijifungia  katika maduka  na bar  zilizopo eneo hilo 
kabla ya  polisi  kuwafuata na  kuwakamata   huko  walikojificha na   
kuwaacha   wale  waliokimbilia msibani .


Kamanda  
wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza  kupatikana   
kuzungumzia tukio  hilo  huku idadi ya vijana  waliokamatwa  kwa tuhuma  
za  kuhusika katika  vurugu  hizo zaidi ya 20  walionekana  wakipagiwa  
katika magari  ya  polisi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)