Pages

Ongezeko la Utalii wa kimatibabu nchini India

Mapema wiki hii dunia iliungana kuadhimisha Siku ya Afya Duniani, kimataifa ni siku ambayo huadhimishwa tarehe 7 Aprili kila mwaka. Siku hii imekuwa ikienda sambamba na masuala ya kiafya na mambo mengine mbalimbali yanayotambua hatua zinazochukuliwa na sekta ya afya katika kupambana na magonjwa. Katika miaka ya hivi karibuni mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakifanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa huduma ya afya ili kuendana na viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Ulaya na Marekani.

Mabadiliko hayo yamesababisha uhitaji mkubwa wa huduma bora hasa kwa watu binafsi kutoka nchi ambazo hazina uzoefu au azijapata mabadiliko. Katika maeneo mengi ya nchi hizo mabadiliko haya na maendeleo ya kiafya yameunda sekta ya aina yake ijulikanayo kama utalii wa kimatibabu (medical tourism) ambapo watu kutoka mataifa mengine husafiri kwenda nchi maalum kwa sababu za matibabu.

Mabadiliko katika ubora wa huduma ya matibabu yamekuwa na matokeo makubwa katika sekta ya utalii wa kimatibabu. Moja ya nchi zilizo mbele katika mabadiliko ni India, ambayo inachangiwa na ukuaji mkubwa wa uchumi katika miaka ishirini iliyopita. India inatambulika kama moja ya nchi inayopendelewa na watu duniani kwa matibabu ya kina zaidi.

Kama taifa linaloendelea gharama zinazotakiwa kwa ajili ya matibabu ni nafuu kulinganisha na mataifa yaliyoendelea. Hii inawezeshwa na ukuaji wa miundombinu na vifaa pamoja na teknolojia ya hali ya juu inayo ifanya India iwe sambamba na maendeleo yaliyopo Marekani au Ulaya. Inakadiriwa kuwa mgonjwa kusafiri kwenda India kwa sababu za matibabu unaweza kuokoa 70-75% ya jumla ya gharama bila kujali anakwenda kwa ajili ya aina gani ya matibabu. Chama cha madaktari wa Marekani (American Medical Association) hivi karibuni kilifanya utafiti juu ya gharama zinazotakiwa kwa ajili ya upasuaji mbalimbali na matokeo kuonyesha kuwa India ina gharama ndogo za matibabu, mara tatu chini ukilinganisha na nchi za magharibi na bado ni kiasi kidogo ukilinganisha na mataifa mengine ya Asia. Kuchukua mfano wa upasuaji wa goti katika maeneo mbalimbali, wastani wa  gharama ni dola 40,000 katika hospitali za Marekani, dola 10,000 katika hospitali za Thailand lakini  India gharama ni dola 8,500. Kadhalika kwa utaratibu kama vile kupandikizwa uboho nchini Uingereza gharama ni wastani wa dola 400,000, dola 150,000 Marekani ambapo India ni dola 30,000.

Tanzania ni moja ya mataifa ambayo inafaidika kutokana na ukuaji wa sekta ya afya na uchumi nchini India, ongezeko la wanaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya huduma za matibabu kwa kiasi kikubwa linaonyesha watu wanapendelea kuchagua hospitali za India. Ongezeko hili la watu halijachukua mkondo mmoja kwa kuwa taasisi mbalimbali zimezingatia mwenendo huu na zimechukua hatua zaidi kuimarisha uhusiano huu. Shughuli za mara kwa mara kama vile madaktari kutembelea Tanzania kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali katika kutoa mafunzo kwa madaktari Watanzania na kliniki za ushauri umejenga sifa ya taasisi ya afya ya India. Kwa kufanya hivyo, imetoa uwezo wa kushinda moja ya vikwazo vikubwa vya utalii wa kimatibabu ambavyo huwa ni vigumu kwa wagonjwa wengi kuweza kulipia gharama za msaada zaidi wa matibabu pindi wanaporudi katika nchi zao.

Miongoni mwa taasisi zinazofurahia uhusiano mzuri na Tanzania ni Hospitali za Apollo. Ikiwa na majengo kadhaa nchini India, hospitali hio imekua na uhusiano mzuri na wakuaminika kwa zaidi ya miaka 12 Tanzania. Kwa kuchochewa na gharama za chini na uwepo wa vifaa, wengi wamechukua fursa hii kama njia ya kukwepa gharama kubwa ya kwenda mahali pengine. Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuvutiwa na hali nzuri ya huduma za afya zinazopatikana katika Hospitali za Apollo, mwaka 2003 kwa udhamini wa serekali kundi la watoto 20 waliohitaji upasuaji wa moyo walipelekwa katika Hospitali ya Apollo Hyderabad. Vituo vya Apollo ziko katika miji mikubwa kadhaa na zimekuwa zikivutia zaidi ya mataifa 150 mbalimbali ambazo zaja kufanya ziara India kila siku. Vituo vya kisasa vya Apollo mjini Apollo Delhi, Hyderabad, Chennai, Ahmedabad na Bengaluru ni miongoni ya zile ambazo zinafahamika kwa kuvutia idadi kubwa ya wagonjwa wa nje.

Taasisi ya Apollo inajivunia kuwa waanzilishi wa huduma bora na maendeleo yake ikisababisha wapate tuzo mbalimbali. Miongoni mwa tuzo za juu ni ile ya Tume ya Pamoja ya tuzo za kimataifa (the Joint Commission International Accreditation (JCI)) ambayo ni kwa ajili ya hospitali zenye lengo la kuboresha ubora wa huduma ya afya na usalama duniani kote. Katika hatua kipekee hospitali zake za mjini Delhi, Chennai, Hyderabad, Ludhiana, Bengaluru, Kolkata, Mauritius na Dhaka zimefanikiwa kupata tuzo hiyo. Na zaidi kituo chake cha Indraprastha Apollo Delhi kiliweka historia kwa kuwa hospitali ya kwanza nchini India kwa kupata tuzo ya JCI mara 4 mfululizo. (i)

Kitovu cha utalii wa kimatibabu ni Jiji la Chennai ambayo inajulikana kam mji mkuu wa kimatibabu nchini India. Ni nyumbani kwa hospitali mbalimbali maalum na inakadiriwa kuvutia wagonjwa 200 kila siku na 45% ya utalii wa kimatibabu katika nchi hiyo. (ii)

Jiji la Chennai linafurahia uhusiano mzuri na Afrika Mashariki, ina mkataba na Serikali ya Tanzania, Kenya na Uganda ili kuhakikisha wananchi wanaohitaji tiba nje ya nchi wanapelekwa Chennai kwa ufadhili wa serikali. Hili limekuwa na ufanisi katika kukuza sekta ya utalii wa kitabibu Jijini hapo.

Wasiwasi kuhusu ubora wa tiba katika nchi zinazoendelea kama vile India umekuwa ukijitokeza, hata hivyo ni muhimu kutambua kwamba wataalamu wengi katika nchi hizi wamepata mafunzo katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani na Uingereza, na hivyo matokeo ya matibabu ni yanayolingana. Madaktari wenye sifa kitaaluma hufanya kazi katika hospitali zilizotunukiwa tuzo mbalimbali si tu katika kutoa huduma za kuaminika lakini pia kwa sukuma mipaka ya huduma za matibabu pamoja na kuja na mbinu za kimapinduzi kufikia viwango vya kimataifa.

Taasisi kama vile hospitali za Apollo hutumika kama ishara ya maendeleo, ikiwa imetokea chanzo kidogo hadi kuwa moja ya watoaji wakubwa wa teknolojia ya juu ya afya pamoja na vifaa bora na vya kisasa sambamba na nchi za Ulaya na Marekani. "Hospitali za Apollo ilifungua milango yake mwaka 1983 na kuleta ubora wa kimataifa wa afya nchini India, kwa gharama iliyoko chini mara kumi unapolinganisha na nchi za Magharibi. Hii ilikuwa mara ya kwanza Apollo kuwajibika kijamii na sasa imekuwa moja ya watoaji wakubwa duniani wa teknolojia ya huduma za afya katika viwango vya dunia ya tatu" anasema mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dr. Prathap .C. Reddy.

Sekta ya matibabu nchini India imetoka mbali katika miongo hii miwili hadi mitatu nyuma, akitoa maoni juu ya mabadiliko haya Dr Prathap c. Reddy alilinganisha sekta ya matibabu ya miaka ya nyuma India na ile ya Tanzania leo na kusema kuwa "chati ya Kujifunza kwa India inaweza kutumika kama jukwaa kwa ajili ya mataifa mengi ikiwa ni pamoja na Tanzania kufikia hadi viwango vya kimataifa vya huduma za afya” anasema kwamba "miundombinu ya sasa na teknolojia inayotolewa katika maeneo kama Tanzania ni miaka 20 nyuma ukilinganisha na dunia nzima" ikiwa ni wito kwa serikali na taasisi binafsi kushinikiza mipaka ya huduma za matibabu kama wenzao kwa nia ya kuiweka Tanzania kama nchi yenye ubora na yenye nguvu katika sekta ya afya ukanda wa mashariki ya Afrika na zaidi.

Kuhusu hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na  utafiti kwa ajili ya jamii  ya kibinadamu".

Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.

Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120. Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710. Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba. Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.

Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)