Pages

News Alert:Jenerali Buhari ndiye rais mpya wa Nigeria

Rais mteule wa Nigeria Buhari
Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na kumuondoa rais aliyeko Goodluck Jonathan mamlakani.
Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha mpigia simu mpinzani wake Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.
Hii ndiyo mara kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.
Goodluck amekiri kushindwa katika uchaguzi huo ulioshuhudia ushindani mkali
Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.
Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile kimajimbo .
Wanigeria wengi wamefurahi kushiriki uchaguzi uliomtoa mamlakani raisl aliyekuwa hatekelezi wajibu wake
Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye wameweza kuing'oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake kikamilifu.
Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)