Pages

Ndesamburo atangaza kuachia kijiti katika uchaguzi ujao

Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakifuatili mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika katika eneo la soko la Manyema.
Katibu mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi na Diwani wa Kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akizungumza katika mkutano
huo wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akiwasili katika viwanja
eneo la soko la Manyema akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Mji Mpya ,Abuu Shayo na Stephen Ngasa wa kata ya Kiusa.
Mstahiki Meya a manispaa ya Moshi,Jafary Michael akihutubia mamia ya wananchi waliofika katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vilivyoko jirani na soko la Manyema .
Mmoja wa wafuasi wa Chadema akiwa amekaa chini akifuatilia mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Philemoni Ndesamburo akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Clement Kwayu wakati wa mkutano wa hadhara.
Mamia ya wananchi katika mji wa Moshi wakishangilia hotuba iliyokuwa
ikitolewa na Msathiki Meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimtambulisha Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge
katika jimbo hili wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
Ndesamburo akizungumza na wananchi wa Moshi mara baada ya kumtangaza mrithi wake katika jimbo la Moshi mjini.
Mamia ya wananchi wakimsikiliza Ndesamburo.
Mstahiki Meya ,Michael akiwa amekaa kando ya Mbunge ,Philemoni
Ndesamburo . Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)