Pages

Mbio za ngorongoro Marathon kufanyika April 18

Waandaaji wa mbio za kimataifa za Ngorongoro Maratahoni katika mkutano na wanahabari kuzungumzia maandalizi ya mwisho ya mbio hizo zinazotarajia kufanyika Aprili 18 mwaka huu ,Karatu mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania Adventure na Zara Charity,Zainab
Ansel akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambazo zinadhaminiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Zara Charity.
Mratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni Meta Peter akizungumzuia wanariadha wa Tanzania ambao wanartarajia kushiriki Mbio
hizo huku akisema mbio za mwaka huu zitashirikisha wanariadhanwalioshiriki mbio za dunia za Nyika mwaka huu watakao toana jasho na wakimbiaji kutoka nchini Kenya,Uganda na Malawi.
Muongozaji wa Mbio hizo kutoka kampuni ya Zara Tour ,Frances
Kilawe akizungumza historia ya Mbio hizo.
Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Zara Charity
Datus Mmary akizungumzia lengo la mbo hizo ambao awali ilikuwa ni
kuchangia katika kutokomeza Marelia na mbio za mwaka huu zitakuwa ni
kwa ajili ya kuchangia elimu hasa kwa watoto wa jamii ya
wafugaji.
Mwakilishi wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Leonard Makule
akizungumzia juu ya udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za kimataifa
za Ngorongoro Marathoni 2015.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)