Klabu ya Manchester united haiko katika kiwango kizuri kwenye ushindani wa klabu za ligi kuu ya England na sasa inaanza kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao.
Habari mpya kutoka ndani ya klabu hiyo ni kuhusu mchezaji wao Robin Van Persieimesema ipo tayari kumpa ofa ya pauni milioni 5 ili aihame klabu hiyo msimu huu.
Mkongwe huyo mwenye miaka 31 amebakiza miezi 14 ili amalize mkataba wake na klabu hiyo ambayo kwa wiki imekuwa ikimlipa 250,000.
Pamoja na klabu hiyo kutaka kumtema vigogo wa Italy Juventus na Inter Milan ziko katika harakati za kutaka kunasa saini ya nyota huyo raia wa Uholanzi huku Man U ikiwa tayari kumlipa nusu ya mshahara huku mwingine akilipwa na klabu ambayo itakuwa tayari kumchukua.
Van Persie amekuwa akiandamwa na majeruhi kwa muda mrefu lakini ameisaidia Man U kufunga magoli 10 katika ligi kuu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)