Pages

KLABU YA MICHEO YA RIADHA YA DAR ES SALAAM ‘DAR RUNNING CLUB’ YAANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA MARATHON 02 MAY 2015


Klabu ya michezo ya riadha ya Dar Es Salaam “Dar Running Club” (DRC) imeandaa mashindano  ya  mbio yajulikananyo kama “Mayday marathon” yatakayofanyika tarehe 02 Mei 2015 yatakayoanza na kumalizika katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay (Police Officers Mess). Mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania  Inspekta Generali wa Police Ernest Jumbe Mangu (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari Mlezi wa Klabu ya DRC Mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni bwana Camillus Wambura) amesema DRC ni klabu ambayo ilianzishwa rasmi kutokana na makundi mawili tofauti yenye malengo sawa kimichezo, yaani Kinondoni police jogging club kutoka Polisi mkoa wa Kinondoni na Dar Es Salaam Athletic Club yenye washiriki kutoka maeneo mbali mbali ya Dar Es Salaam wakaamua kuungana na kuwa DRC. 

DRC ina madhumuni makubwa  ya kuendeleza michezo ya riadha nchini mpaka nje ya nchi na kuhimiza afya njema kimwili na kiakili, lakini pamoja na hayo muungano huu wa klabu unasaidia sana kuimarisha mahusiano  kati ya  Polisi na raia, hii inasaidia sana katika usalama na kukuza na kuendeleza dhana ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa jamii. Aliongezea…
 
Naye Captain wa DRC bi (Stella Mandago, na mratibu wa mashindano haya amesema kuwa Mashindano haya yanatarajia kushirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka hapa nchini na  nje ya nchi pia, mashindano haya yatakuwa na washiriki watakao shiriki katika mbio za kilometa ishirini na moja nukta moja (21.1km) na kilomita kumi (10.0Km) yakiwa na lengo la kukuza na kuendeleza michezo ya riadha Tanzania na nje ya nchi ili kuwawezesha wanamichezo kufikia hatua za kimataifa na kuhimiza
maisha yenye afya pia kudumisha mahusiano baina aya police na jamii.

 Klabu ya michezo ya Riadha “Dar Runing Club” inachukua fursa  hii kukukaribisha kushiriki mbio hizi zinazotarajiwa kuanza majira ya saa kumi na mbili asubuhi 12:00 katika viwanja tajwa hapo juu,
aliongezea…..

Kutakuwa na zawadi kwa washindi kumi wa kwanza kwa wanawake na wanaume kama ifuatavyo kwa nusu marathoni ya km 21

 Mshindi wa kwanza  TZS 1,100,000
Mshindi wa pili   TZS 800,000
Mshindi wa tatu TZS 600,000
Mshindi wa nne TZS 350,000
Mshindi wa tano TZS 300,000
Mshindi wa sita TZS 250,000
Mshindi wa saba TZS 200,000
Mshindi wa nane TZS 1500,000
Mshindi wa tisa of TZS 100,000
Mshindi wa kumi of TZS 50,000

Kutakuwa pia na washindi wa 3 kwa mbio za Km 10 kama ifuatavyo

Mshindi wa Kwanza  TZS 500,000
Mshindi wa PIli  TZS 300,000
Mshindi wa tatu  TZS 200,000

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)