Pages

Kivumbi leo UEFA, Bayern,PSG kufa kupona


Luis Suarez mfungaji wa mabao mawili ya Barcelona ilipoilaza Paris Saint Germain 3-1
Kindumbwendubwe cha mzunguko wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali kinarindima tena Jumanne usiku kwa timu ya Paris Saint Germain kupambana na Barcelona katika dimba la Camp Nou.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wiki iliyopita timu hizo zilipambana mjini Paris kwa Barlena kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.
Mfungaji mkubwa wa magoli wa timu ya Paris St-Germain, Zlatan Ibrahimovic atakuwepo katika mchezo wa Jumanne timu yake itakapovaana na Barcelona.
Zlatan Ibrahimovic atakuwa katika kikosi cha PSG baada ya kukosa mchezo wa kwanza mjini Paris wiki iliyopita.
Ibrahimovic, hakucheza timu yake ilipobamizwa mabao hayo 3-1 kutokana na adhabu aliyokuwa akitumikia, lakini katika mchezo wa Jumanne kama ilivyo kwa mchezaji kiungo wa timu ya PSG,Marco Verratti. watakuwa katika kikosi cha timu yao kujaribu kubadili matokeo ya mchezo wa kwanza wa wiki iliyopita mjini Paris.
Luis Suarez - mfungaji wa magoli mawili kati ya matatu atashirikiana na Messi pamoja na Neymar kusaka magoli zaidi watakapokuwa nyumbani Camp Nou.
PSG itamkosa nahodha wake Thiago Silva kutokana na kuwa majeruhi. Nafasi yake ilichukuliwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea Chelsea David Luiz.
PSG inahitaji ushindi wa magoli matatu ili kuizuia Barcelona isiweze kusonga mbele nusu fainali.
Mchezo mwingine utakaovuta hisia za watazamaji ni ule kati ya Bayern Munich dhidi ya FC Porto. Katika mchezo wa wiki iliyopita, FC Porto alitumia vyema uwanja wake na kupata ushindi wa mabao 3-1.
Bayern ina kibarua kizito itakapoikaribisha FC Porto katika dimba lake la Allianz Arena.
Timu zitakazofuzu hatua hiyo zitaingia nusu fainali.BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)