Pages

Kampuni ya coral paints katika jitihada za kuongeza ujuzi kwa wapiga rangi nchini Tanzania



Ili kuwa mpiga rangi mzuri na mpambaji , lazima mtu awe mbunifu na mwenye ujuzi unaostahili vilevile awe na uwezo wa kuelewa  na  kufuzu ujuzi  wote unaohitajika katika kudumisha kiwango cha hali ya juu katika sekta ya upakaji rangi na mapambo . Kwa kiwango cha kitaifa sekta ya upakaji rangi imepata kuungwa mkono ili kuongeza ujuzi kwa maelfu ya wafanyabiashara nchini. Ukosefu wa maarifa na ujuzi muhimu kwa watu wanaopaka rangi umekuwa ukisababisha msuguano kati ya wamiliki wa nyumba , makandarasi na sekta ya rangi kwa ujumla. Hii imesababisha mara kadhaa kutupia lawama kimakosa kwa wauzaji wa  bidhaa hizi badala ya wapaka rangi wenyewe . Mbinu mbaya za upakaji rangi, njia ya mkato  katika kazi na uchaguzi mbovu wa matabaka  ni miongoni mwa sababu zinazochangia viwango vibaya vya kazi.

Kwa kutambua kiwango cha uwezo miongoni mwa wapaka rangi nchini Tanzania, kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa rangi ya  Coral Paints imechukua hatuakatika kuinua viwango vya ujuzi kwa wapaka rangi katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwahimarisha zaidi katika kazi zao. Mpango huo ambao ulianzishwa na kampuni hiyo mwaka 2003 umekuwa jukwaa kubwa kwa ajili ya kuinua elimu na ujuzi nahivyo kuwanufaisha watanzania kiujumla. Kutokana na takwimu za sasa , kuanzia mwaka 2003 hadi sasa kampuni imeendesha madarasa zaidi ya 2,000 kwa ajili ya kutoa elimu hiyo,  na kufanikiwa kuwapatia mafunzo zaidi ya wapaka rangi 100,000.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Coral Paints, Mheshimiwa Kishan Dhebar , wamegundua kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa mafunzo hayo kwa ajili ya wapaka rangi. Anasema, " Baada ya kugundua ujuzi unaotakiwa katika mchakato wa upakaji rangi ni dhahiri kuwa kuna ukosefu wa ujuzi huo ndani ya nchi, na hivyo basi tulionani vema sisi kama shirika linaloongoza katika soko la rangi kujenga jukwaa lambalo litawasaidia wapakarangi  kupokea mafunzo ya kutosha ambapo sio tu wao watakaofaidika nayo lakini ni sekta nzima kwa ujumla. Kama sekta ya rangi inavyozidi  kukua ndivyo pia mahitaji ya wafanyabiashara wenye ujuzi wanaongezeka. Hii imesababisha kuingia katika eneo ya watu ambao hawana elimu ya awali ya biashara kuanza mazoezi na mafunzo madogo sana "Bw Kishan anaendelea kuongeza kwamba " ingawa tunatoa fursa za ajira ni muhimu pia kuandaa vijana wenye ujuzi ambao hauta haribu ubora wa bidhaa zetu kwani kupitia shughuli kama hizi sekta hii inahitaji kupata sifa inayostahili.

Coral Paints hawajaweka mipaka ya mafunzo yao kwa watanzania pekee , bali wametekeleza mkakati huu  katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo kwa bidhaa zao nyingi ndani ya masoko hayo. Mwaka 2014 peke yake jumla mafunzo 175 yamefanyika nchini Tanzania , Malawi na Zambia ambapo mwaka 2015 Februari jumla ya mafunzo 28 tayari imefanyika katika mikoa na nchi jirani. Katika shughuli zote hizi jumla ya wapaka rangi 3,778 walipewa mafunzo yahusianayo na rangi. 

Mafunzo hayo huhusisha mada zinazogusa sekta ya rangi  kwa ujumla. yanahusisha masuala ya msingi kama vile rangi ni nini, faida, viungo, kuoanisha rangi , aina tofauti ya nyuso sifa zake na mbinu ya upakaji rangi. Mafunzo hayo pia hutumika kama jukwaa la kushughulikia malalamiko yanayojitokeza juu ya bidhaa flani, huanzishwaji wa bidhaa mpya, mbinu mbalimbali na hatua za usalama .

Muhitikio kutoka kwa wapaka rangi kwa ajili ya mafunzo hayo umekuwa chanya; Kwa zaidi ya miaka sasa  yameonekana kuwa muhimu katika kuinua kiwango cha uelewa miongoni mwa Wasanii juu ya masuala mbalimbali. Mafunzo hayo pia yamekuwa na thamani ya fedha kwa Wasanii kama mbinu kufundishwa kuwaruhusu kuwa na ufahamu zaidi juu ya gharama zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupunguza kesi na makosa yaliyokuwa yakijitokeza.  Utoaji wa vyeti kwa washiriki  mwishoni mwa mafunzo  kutoka kampuni ya Coral Paints umenufaisha  watu wengi katika kupata ajira.

Coral Paints inatarajia  kuhakikisha kwamba viwango bora vya rangi ambavyo wao utengeneza  vinatumika kwa ustadi na mtu aliye naujuzi na elimu ya kutosha ili kufikia matokeo bora iwezekanavyo kwa namna ambayo ilikuwa lengo lao kubwa wakati wa uzalishaji wa bidhaa hizo. Kampuni ina nia ya kuendeleza mafunzo haya kwa wapaka rangi mbalimbali nchini na kutoa ushauri sitahiki juu ya jinsi ya kufanya zaidi nje ya taaluma yao. Hatua kama hii wakati huu wa mabadiliko chanya lazima ipongezwe na kuwa mfano wa kuigwa ili kuhakikisha sekta inaendelea katika mwelekeo sahihi.

Kuhusu Insignia
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.

Hivi leo, Insignia imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini  Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini  Tanzania umewezeshwa na  ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini  Uingereza na Pat’s Deco ya  Ufaransa.

Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza  rangi na  bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada  mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatngenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo  na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni  bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoedana na thamani- ya -fedha.

Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora wake.  Viwanda vyake vina  vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa.
Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na  Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.



No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)