Pages

HOSPITALI ZA APOLLO KUHIMIZA WAGONJWA WA HAEMOPHILIA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Kujikata, kugongwa na kuchubuka ni ajali za kawaida kwa watu wengi sababu ya shughuli za kila siku, nyumbani na sehemu nyingine ajali hizi hazikwepeki na mara nyingi hazitiliwi mkazo kiafya. Hata hivyo kwa watu wenye haemophilia ajali kama hizo ndio sababu kubwa ya kutufanya kuchukua tahadhari zaidi. Ugonjwa huu kwa kiasi kikubwa ni wa kimaumbile na unadhoofisha uwezo wa mwili kujikarabati wenyewe wakati unapoumia kwa kujikata au michubuko. Taasisi mbalimbali zimekuwa zikijaribu kuongeza uelewa zaidi juu ya ugonjwa huu, kimataifa Siku ya haemophilia duniani inaadhimisha kila mwaka tarehe 17 mwezi wa Aprili.

Mwili wa binadamu kwa kawaida unajilinda wenyewe kupitia mchakato wa ugandishaji damu unapojikata au kujichubua kwa bahati mbaya. Chembechembe za kugandisha damu hujitokeza juu ya ngozi kuzuia kutoka kwa damu, baada ya chembechembe za kugandisha damu kuziba sehemu iliyodhurika, zinatoa kemikali ambazo zinatoa gundi na kuamsha protini mbalimbali kwenye damu zijulikanazo kama vigandisha damu. Protini hizi zinachanganyika na chembechembe za kugandisha damu kuunda nyuzi, na nyuzi hizi hufanya matone ya damu kuganda. Hali hii ni tofauti kwa watu wanaoishi na haemophilia; haya ni majeraha madogo madogo yanayoweza kusababisha kuvuja damu kukadumu kwa muda wa siku kadhaa au wiki kadhaa, au isitibike kabisa. Wakati mwingine watu wa aina hii hupatwa na tatizo la damu kuvuja ndani kwa ndani katika sehemu kama magoti, vifundo na viwiko hali hii huhatarisha uhai ambapo kuvuja kwa damu kunasababisha kuharibika kwa viungo na tishu za mwili.    

Kulingana na Dkt. Anoop P, Mshauri wa Haemotolojia na Upasuaji wa Saratani kwa Watoto katika Hospitali za Apollo, Bangalore, Haemophilia ni ugonjwa wa  kuvuja damu unaorithiwa na unaosababisha kushindwa kuganda kwa damu. Unasababishwa na kushindwa au kukosekana kwa moja ya protini za kugadnisha damu iitwayo Factor VIII (Haemophilia A) Au Factor IX (Haemophilia B) kwenye damu.

Anasema kuwa “tabia ya watu wenye Haemophilia zinatofautiana kulingana na ukubwa wa kasoro katika jeni. Kuvuja kwa damu hakutakuwa kwa kasi ila ni kwa muda mrefu kuliko watu wa kawaida. Kwa kesi ndogo na za kawaida za Haemophilia, kuvuja damu kunatokea baada ya kujeruhiwa au upasuaji, lakini katika hali mbaya zaidi ya Haemophilia kuvuja kwa damu kunatokea katika maungio na misuli. Dalili zinazoelezea kuvuja damu kwa ndani ni pamoja na uvimbe, maumivu makali, joto, kushindwa kujongea na kusogeza miguu. Wakati wowote inapotokea kuvuja kwa damu ndani, wagonjwa wa haemophilia wanapaswa kuwekwa katika hali isiyochochea kuendelea kuvuja kwa damu na kujitahidi kuzuia kuvuja kwa damu ikifwatiwa na mazoezi ya kina kurejesha utendaji wa kawaida wa maungio na misuli”

Inashauriwa kuwa watu walioathirika na Haemophilia wafanye mazoezi maalumu kuimarisha maungio, hasa viwiko, magoti na vifundo. Mazoezi yanaongeza wepesi wa mwili na kuimarisha misuli, kuongeza uwezo wake wa kulinda maungio yasidhuriwe kwa kuvuja kwa damu. Mazoezi haya yanashauriwa kufanywa inapotokea kuvuja kwa damu na pia kila siku ili kuimarisha misuli na maungio kuzuia kuendelea kwa matatizo ya kuvuja kwa damu.

Kwa kuzingatia mzigo unaosababisha kuteseka kwa hali hii Dkt. Anoop P, Mshauri wa Haemotolojia na Upasuaji wa Saratani kwa Watoto katika Hospitali za Apollo, Bangalore anaelezea ratiba ya kila siku ya mazoezi na anashauri kuwa sanduku la vifaa tiba vya mazoezi nyumbani kuendeleza na kuimarisha misuli ipasavyo ili kuzuia na kupunguza kujirudia kuvuja kwa damu.

Sanduku linakuwa na jozi ya mipira ya kuvutika, mifuko ya mchanga yenye zipu, raba bendi zenye uwezo tofauti tofauti. Kwa vifaa vichache tu watu wanaweza kufanya mazoezi mbalimbali yanayolenga maeneo ya msingi yenye matatizo. Makundi hasa ya misuli ambayo mazoezi moja kwa moja yanalenga ni pamoja na mikono, viganja, mabega, misuli ya nyonga, misuli ya mikono, misuli ya paja, viwiko na mikujo.

Mazoezi ya mpira ni maalum kwa misuli ya mikono na mabega. Wakati wa mazoezi mtu anatakiwa kushikilia mipira laini, kuiminya kwa kubana misuli ya juu ya mkono. Itaimarisha misuli yote ya mkono, kiganja, mishipa ya mkono na bega.

Mazoezi ya mifuko ya mchanga ni maalum kwa kuimarisha misuli ya nyonga. Mgonjwa anatakiwa kukaa kwa kujiachia juu ya kiti chenye kiegemeo. Kisha kuweka mfuko wa mchanga juu ya mapaja, nyanyua miguu juu kwa kukunja nyonga. Hii inasaidia kuzuia kujirudia kuvuja kwa damu katika misuli ya mapaja kwa kuimarisha misuli ya nyonga. Katika kuimarisha misuli ya paja, mtu akae kwa kujiachia kwenye kiti chenye kiegemeo na aweke mfuko wa mchanga kwenye vifindo vya miguu. Kwa kunyanyua miguu huku magoti yamenyooka inasaidia kuimarisha magoti na kujongea kwake kwa kuimarisha misuli ya paja.

Mazoezi ya raba bendi yanafanyika kuimarisha misuli ya nyuma ya mkono. Mgonjwa ashike raba bendi; aivute kwa kuitanua huku amenyoosha kiwiko. Hii inasaidia kuzuia na kurekebisha mkunjo wa mkono kwa kuimarisha misuli ya nyuma ya mkono. 

Kuimarisha misuli ya nyuma ya paja inafanyika kwa kukaa kwenye kiti chenye kiegemeo. Mgonjwa anatakiwa kuweka mguu katikati ya raba bendi ambayo imawekwa katika kona ya kitu kizito.  Tanua raba bendi kwa kukunja goti. Hii inasaidia kuimarisha goti kwa kuimarisha misuli ya nyuma ya paja.
Wagonjwa wanaweza kuimarisha vifundo vya miguu na mijongeo yake kwa kuimarisha ugoko wa mbele ya mguu na misuli yake kupitia kuimarika kwa magoti. Mgonjwa akae kwenye kitanda anyooshe miguu. Weka raba bendi kwenye kanyagio; tanua bendi kwa kunyanyua mguu juu. Uimara zaidi kwenye eneo la vifundo unapatikana kwa kukunjwa na kukunjua maungio, ambapo mtu amekaa kwenye kitanda na miguu ikiwa imenyooka. Anaanza kwa kuingiza mguu kwenye raba bendi na kuishikilia kwa makini kutumia mkono kisha tanua bendi kwa kusukuma mguu chini. Hii inasaidia kuzuia misuli kuvuja damu na kuimarisha vifundo nya maungio.

Dkt. Anoop P anamalizia kusema “kwa wagonjwa wa haemophilia, kujirudia kuvuja damu katika viungo na misuli ileile inasababisha uvimbaji kwa viungo na misuli. Mara nyingi hii hutokea kwenye magoti, viwiko, vifundo na misuli inayolengwa ni ile ya nyonga na misuli midogo. Utaratibu mzuri wa mazoezi uhimarisha zaidi misuli na maungio na hivyo basi kumsaidia sana mgonjwa wa haemophilia”.



No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)