Pages

Hospitali ya Apollo kuendesha kambi ya uchunguzi kwa ajili ya wagonjwa wa Moyo na mfumo wa fahamu Tanzania

Dar es Salaam: Mwezi  Machi sekta ya afya nchini Tanzania imepokea wataalam kutoka nchi  mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa huduma za vipimo, ushauri na matibabu kwa watanzania. Ujio huu umeleta faida kubwa kwa wagonjwa na wataalamu nchini. Miongoni mwa waliotembelea ni timu ya Madaktari bingwa  kutoka Israel na Hospitali za Apollo zilizopo nchini India. Ziara hizi za mwishoni mwa mwezi March zilitanguliwa na ziara ya madaktari wawill kutoka hospitali ya Apollo ya bangarole mwanzoni mwa mwaka huu.

Ikiwa tayari walifanya kliniki ya ushauri kwa ajili ya wagonjwa wa figo na mfumo wa fahamu timu ya wataalam kutoka hospitali ya Apollo Bangalore ilirudi Tanzania kwa ajili ya uchunguzi na kutoa ushauri zaidi kwa  wagonjwa wa Moyo na mfumo wa fahamu. Kliniki hiyo ilifanyika mwishoni mwa Machi katika hospitali ya Medi Ed jijini Dar es salaam, iliandaliwa na Dk. Girish Navasundi, dakitari mwandamizi wa magonjwa ya moyo, katika hospitali ya Apollo ya Bangalore na Profesa Dk Krishna Kambadoor, Mkurugenzi wa Taasisi ya sayansi ya mfumo wa fahamu kutoka Hospitali ya Apollo ya Bangalore. Kliniki hiyo ilitoa fursa kwa umma kupata uchunguzi wa matatizo hayo bure bila kulipia gharama yoyote na pia kuruhusu madaktari kufuatilia maendeleo ya wagonjwa wao ambao  hawakuweza kurudi india kwa uchunguzi na matibabu ya zaidi.

Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza (NCD)  kama vile moyo, mfumo wa neva na mgongo yamekua  yakiongezeka kwa kasi na kusababisha  ongezeko la vifo nchini. Akizungumza na waandishi wa habari wakati madaktari kutoka Israel wakiwafanyia uchunguzi watoto wenye matatizo ya moyo, makamu  Raisi wa chama cha madaktari wa watoto Tanzania, Dk Namala Mkopi alizungumzia matatizo ya magonjwa ya moyo kwa jamii na hasa kuonyesha athari zake kwa watoto wachanga na kusema kuwa inakadiliwa "watoto 13,600 nchini huuzaliwa na  matatizo ya moyo kila mwaka na asilimia 25 tu ndio wana uwezo wa kupata matibabu. Mwaka 2013 na 2014 kati ya watoto 322 waliokutwa na matatizo, 128 tu walipata nafasi ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi"

Wakati wa wakati wa kambi ya uchunguzi iliyooandaliwa na  Hospitali ya Apollo, Dr Girish B Navasundi dakitari mwandamizi wa magonjwa ya moyo, katika hospitali ya Apollo ya Bangalore aliwahudumia wangonjwa wenye magonjwa yanayohusiana na moyo. Dr Girish B Navasundi ni dakitari bingwa na mashuhuri kwa kuwa na uzoefu mkubwa wa miaka kadhaa katika idara ya magonjwa ya moyo, baada ya kufanya zaidi ya matibabu ya moyo kwa wagonjwa 1700 kwa njia ijulikanayo kitaalamu kama Angiograms. Zaidi ya mafanikio haya pia anatambulika kwa kufanya matibabu ya moyo kwa wagonjwa 350 kwa njia ijulikanayo kitaalamu kama Angioplasties.
Katika Kambi hiyo  Dk Navasundi alikuwa na nafasi ya kuelimisha Watanzania juu ya umuhimu wa maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa ya moyo utamaduni ambao Watanzania wengi hawana. Alisema kuwa, "moyo hauwezi kufanya kazi bila maji ikiwa asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Kwa hiyo, unywaji wa maji ni muhimu kwa  utendaji wa mwili, na hasa zaidi kwa  mishipa ya moyo"

"Nini kinatokea kama mtu hata kunywa maji? Kwanza, mishipa midogo ya damu (capillaries) katika mwili wako itafunga. Hii kuongezeka upinzani katika mzunguko wa damu na kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu. Ukosefu wa maji  huongeza hatari kwa moyo, kushindwa kwa mshipa ya damu, na matatizo mengine yanayoendana na hayo." alisema.

"Ni kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa?  Mwili wa binadamu unahitaji angalau ml 35 ya maji kwa  kila kilo ya uzito wa mwili kwa siku , ambayo ni sawa na ml 2100  kwa mtu wa uzito wa kg 60. Kutumia glasi tano za maji au zaidi kwa siku kwa kiasi kikubwa hupunguza mashambulizi ya moyo kwa kiasi kikubwa, ikilinganishwa na kunywa chini ya glasi mbili za maji kwa siku "aliongeza Dk Navasundi.

Dk Navasundi alihitimisha kwa kuelezea faida za matumizi ya maji ya kutosha katika kufanya  damu kuwa nyepesi kama inavyotakiwa kuwa, hurahisisha mzinguko wa damu kwenda kwenye moyo, kupungua kazi kubwa ya moyo vile kupunguza hatari ya damu kuganda ndani ya mishipa,.

Tanzania imekua ikifaidika na msaada kutoka jumuiya za Kimataifa, uingiaji wa madaktari mashuhuri kutoka nje imekua si tu faida watu wanaohitaji matibabu lakini pia wataalamu wa hapa nchini kwa sababu  inawapa nafasi ya kupata elimu ya matibabu, tukio ambalo litawanufaisha Watanzania kwa muda mrefu.

Kuhusu Hospitali ya Apollo, Bangalore Idara ya Magonjwa ya moyo
 Idara inalenga katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo  kupitia njia vamizi na zisizo vamizi matibabu na uchunguzi unaosimamiwa na timu ya wataalamu wenye ari na nia ya dhati. Katika idara ya hii kuna timu ya madakitari wa moyo waliojitolea ambao wanafanya kazi sanjari na kutoa huduma kwa kina, kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo. Timu ya madaktari, manesi na wataalamu wengine wa moyo wanakuwepo kuhakikisha ubora katika huduma anayopatiwa  mgonjwa.

Idara ya magonjwa ya moyo katika Hospitali ya Apollo imeadhimia kutoa huduma ya afya ya kiwango cha kimataifa kwa gharama nafuu. Timu yenye utaalamu ya madakitari bingwa wa moyo  pamoja na teknolojia ya kisasa huhakikisha huduma bora kwa wigo mpana wa magonjwa ya moyo.

Pia kuna idara inayohusika na matatizo ya moyo kwa watoto pekee (ikiwa ni pamoja watoto ambao bado hawajazaliwa), waliozaliwa na wanaokua. Miundo, kazi, na matatizo yanayohusiana na magonjwa ya moyo  hushughulikiwa kwa mafanikio ya hali ya juu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)