Pages

Habari za moja kwa moja kutoka Garrisa nchini kenya

Ramani ya chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya
Takriban watu 15 wanaodaiwa kufinika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu hao wanaodaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.
Mwandishi wetu anasema kuwa wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliosalimika
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
13.40pm:Waislamu na wakristo waliotekwa ndani ya Jumba hilo la Chuo kikuu cha garissa wamedaiwa kutawanywa kabla ya waislamu 15 kuwachiliwa huru kulingana na msemaji wa kundi hilo la Alshabaab.
13.35pm:Serikali ya kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihutubia taifa kufuatia shambulizi hilo la chuo kikuu cha Garrisa mapema leo.
13.30pm:Alshabaab:
Maafisa wa Polisi wa kenya
kundi la wapiganaji wa Alshabaab limesema kuwa liko ndani ya Chuo hicho kikuu na limewatawanya waislamu na wakristo
13.20pm:Wapiganaji wamedaiwa kuwateka nyara wanafunzi na kuwaua watu 14 katika chuo hicho kulingana na wafanyikazi wa msaada na maafisa wa polisi.Takriban watu 65 wengine wamejeruhiwa baada ya washambuliaji kuvamia chuo hicho.Vituo vya habari nchini kenya hatahivyo vinaiweka idadi hiyo kuwa watu 16.
13.05pm:Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la wapiganaji wa kundi la alshabaab imefikia 14
13.03pm:Al shabaab
Alshabaab lakiri kutekeleza shambulizi
Kundi la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa Kaskazini mashariki mwa Kenya huku likiwaua watu 14
12.47pm:Wanafunzi
wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya
Chuo hicho cha Garissa kina takriban wanafunzi 1000, na wafanyikazi wengine.
12.30pm Wanafunzi:
Wanafunzi waliodaiwa kutoroka
Baadhi ya wanafunzi wamedaiwa kutoroka kutoka mabweni waliokuwa wakilala
12.20pm:Wapiganaji
Wapiganaji
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la Chuo kikuu .
12.18pm:Kenya Red Cross
Maafisa wa polisi wakikabiliana na wapiganaji huko Garissa kenya
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na majeraha mabaya..Kwa sasa shirika hilo linawasafirisha madaktari katika eneo hilo.
11.30am Idadi ya watu waliouawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya imefikia watu sita huku wengine 29 wakidaiwa kujeruhiwa.BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)