Pages

Clouds fm yashinda tuzo ya Super brand kwa mara nyingine tena

 Picha ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta  ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya  Alliance Insurance.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana  Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds  Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian  Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na  Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi  Fauzia Kullane.
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana  Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji  na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo bora za viwango hizo  iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na Mkuu  wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana  Jawad Jaffer.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa  habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo  iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji  tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe


KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki. Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad  Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya  kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza  makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango  makao makuu nchini   Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko  na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.

Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000
zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands
na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya
jsu  kwa mwaka wa 2015 -2016.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)