Pages

Busara ya madiba funzo kwa wanaharakati na wanasiasa

"BUSARA YA MADIBA NI FUNZO KWA WANAHARAKATI NA WANASIASA WETU".Historia haina uchoyo na mawazo kwa kila mwanadamu aliyejitosa kutengeneza historia.NELSON MANDELA ni miongoni mwa wanahistoria waliowahi kuijua na kuitengeneza historia ya dunia na kuwastaajabisha magwiji wa kihistoria wa huko ughaibuni kama akina Hegel,almond na wengine wengi.Madiba alikuwa ni mwanasiasa aliyeamini kuwa haki itapatikana kwa njia ya amani kabisa(non violence).

Ili kuweza kutimiza ndoto zake za kuwakomboa watu wake,silaha kubwa ilikuwa ni mikutano ya hadhara,machapisho mbalimbali ya magazeti na majalida yaliyobeba dhana ya ukombozi lakini pia aliweza kutumia nguvu kubwa ya kuviunganisha vyama vingine vya kisisa kuwa kitu kimoja vyama kama PAC,ANC viliweza kuungana na kuwa na dhamira ya dhati ya kuwakomboa wana waafrka ya kusini.

Chachu ya ukombozi ilichochewa haswa na azma ya kishetani ya makaburu baada ya kuigawa Afrika kusini kwa namna ilivyo wapa ardhi bora kabisa ya kilimo takribani asilimia 87 walijimilikisha huku asilimia 13 ya udongo mkavu wakiachiwa wamatumbi,wamanyema na wakwere lakini pia makaburu hawa walitenga risavu kwa waafrika kwa kuwatangazia uhuru.Mambo haya yalileta msuguano mkubwa miongoni mwa wazawa,ndipo katika miaka ya sitini Mandela aliunda jeshi la vijana almaarufu UMKHOTO WE SIZWE(mkuki wa taifa). "The spear of nation" Umkhoto we sizwe ni kazi ya wanaume na wanawake pamoja na watoto kwa maelfu waliojitoa mhanga ili kudai nchi ya mababu zao.Hatimaye ukombozi wa afrika kusini uliweza kupatikana pindi De klerk alipotangaza kwamba atakuwa makamu wa raisi chini ya rais mweusi yaani MANDELA.TUMEJIFUNZA NINI KWA MANDELA? Kwanza roho ya kutolipa visasi,baada ya miaka ishirini na saba jela,kwa mtu aliyeteswa kwa muda wote huo wengi walitarajia kuwa kilikuwa kipindi kigumu kwa makaburu lakini aliushangaza ulimwengu kwa kuwasamehe kwa yale yote waliyoyafanya.

Huu ni moyo wa kipekee wanasiasa wetu yawapasa kuuiga PILI Mandela aliendelea kuamini njia sahihi ya ukombozi ni AMANI.Hili ni funzo kwa viongozi wetu kuwa hata Diplomasia ni bora kuliko maandamano na vita.Ushauri kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa,HAKI ni dhana pana na inaweza kupatikana hata kwa AMANI kabisa bila vurugu,maandamano na vitisho viongozi wenye hekma za kidiplomasia kama MANDELA wanatufaa sana kwa mazingira ya sasa TATU Mandela hakuamini katika uchu wa madaraka ndio maana aliongoza kwa miaka minne pekee kwa kutambua dhana ya demokrasia ktk uongozi.

USHAURI viongozi wetu ni lazma wajitambua nni maana ya kuwa ktk uongozi,lakini mbaya zaidi wengine hudhani uongozi ni kuongoza taasisi nyingi,huku unakuta kiongozi wa chama na pengine ni kiongozi wa taasisi,Tujifunzeni kwa madiba NNE na mwisho Mandela aliamini siasa ni jumla na mstakabali wa maisha ya mwanadamu,lakini leo hii uongozi umepoteza maana yake halisi pindi mtu anapokuwa mtaalamu wa uongo,nghiliba na propaganda chafu dhidi ya wengine hujulikana kama wanaharakati. Kuelekea uchaguzi mkuu wa oktaba mwaka huu yatupasa kuwa makini na wanaojiita wanaharakati wanaotumia uelewa mdogo wa wananchi katika siasa,uchumi na dhana nzima ya maendeleo kupata madaraka pia propaganda chafu ndio mitaji yao kisiasa.Tanzania yenye NEEMA tele inawezekana tekeleza wajibu wako wakujiandikisha sasa ili uweze kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae kupiga kura ni haki na wajibu wa kila Mtanzania mwenye sifa kwa mujibu wa katiba

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)