Pages

Amri wafugaji kuwapiga picha ngombe wao

Yeyote atakayechinja atahukumiwa kifungo cha miaka 5 jela
Polisi nchini India wamewalazimu wafugaji wa ngombe kuwapiga picha ilikufanikisha sheria mpya inayoharamisha uuzaji wa nyama ya ngombe.
Maafisa katika mji wa Malegaon, ulioko katika jimbo la Magharibi la Maharashtra wanasema kuwa pich hizo zitasaidia katika kutekelezwa kwa sheria hiyo mpya.
Sheria hiyo imeharamisha kuchinja na kuuza nyama ya ng'ombe kwa mjibu wa jarida la the times.
Ng'ombe hutizamwa na hadhi ya juu kwa misingi ya kidini India
Sheria hiyo ya jimbo la Maharashtra ilianza kutekelezwa Machi tarehe mbili 2 baada ya mjadala uliodumu zaidi ya miaka 19.
" hizi picha tutazihifadhi kisha tutazitumia tu kukiwa na haja ya kutoa ushahidi'' alisema afisa mkuu wa jimbo hilo Mahesh Sawai.
"endapo mtu atamshaki mwenzake kwa kukiuka sheria hizi picha zitatumika kama itibathi ya umiliki wa ng'ombe''.
India:Wafugaji kupiga picha ngombe wao
Polisi walitangaza sheria hiyo mmpya baada ya watu watatu kushtakiwa kwa kuvunja sheria hiyo mpya.
Hiyo ndiyo iliyokuwa kesi ya kwanza chini ya sheria hiyo mpya.
Jimbo hilo la Maharashtra liliharamisha uchinjaji wa ngombe mwaka wa 1976, lakini sheria hii mpya sasa inaharamisha hata kuchinja mafahali ambao kwa kawaida hufugwa kwa ajili ya nyama.
Polisi wanawataka wafugaji wawapige picha ngombe wao
Hata hivyo nyama ya nyati ni halali katika jimbo hilo.
Adhabu ya hukumu ya miaka mitano gerezani inawasubiri wale wote watakaopatikana na hatia.
Haijulikali makataa hayo ya kutochinja ngombe itaathiri vipi idadi ya mifugo ambayo ilisemekana kuwa takriban milioni 21 ukilinganishwa na hesabu ya jumla ya watu milioni 112 kulingana sensa ya mwaka 2012.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)