Pages

YAHOO kufunga ofisi zake China

Yahoo kufunga ofisi zake nchini China
Kampuni ya mtandao YAHOO inatarajiwa kufunga ofisi yake ya mwisho katika eneo la China bara.
Kampuni hiyo kama kampuni nyengine za kiteknologia imekuwa ikikabiliwa na ushindani mkubwa nchini Uchina kutoka kampuni nyengine za mtandao.
Takriban ajira 300 zitapotea.
Yahoo ilisitisha utoaji wa huduma za kutuma ujumbe kwa kutumia njia ya Email kwa wateja wake nchini Uchina mnamo mwaka 2013.
Katika taarifa yake,kampuni hiyo imesema kuwa inaunganisha baadhi ya huduma zake ili kuimarisha ushirikiano.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)