Baadhi ya wanahabari wanaoshiriki katika warsha ya mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) wakiwa katika warsha ya siku mbili jijini Mbeya
Baadhi ya waraghbishi wa ngazi ya jamii kutoka kata ya Msalama wilaya ya Mbeya vijijini wakiwa katika warsha hiyo
Mwezeshaji wa warsha hiyo akiwaonyesha baadhi ya mambo yaliyoibuliwa na waraghbishi wa ngazi ya jamii wilaya ya Mbeya vijijini.
..............................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
WAKATI serikali na wanaharakati mbali mbali wakiendelea kupiga vita mila potofu za kurithi wajane ,baadhi ya wanawake wa kata ya Mlalala wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya wameeleza kusikitishwa na vitendo vya baadhi ya wajane kuendelea kunyanyasika pale wanapokataa kurithiwa .
Hayo yameelezwa leo wa waraghbishi wa jamii katika ngazi ya kijiji kutoka kata ya Mlalala wakati wakielezea matokeo ya tafiti walizozifanya katika vijiji vya kata hiyo .
Akizungumza mbele ya washiriki wa warsha ya siku mbili ya mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) inayoendelea jijini Mbeya kwa kushirikisha wanahabari wa vyombo mbali mbali kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa ,mwakilishi wa waraghabishi hao Bi Huruma Mahenge alisema kuwa hadi sasa tatizo hilo bado ni kubwa zaidi.
Kwani alisema kuwa baadhi ya wanawake wameendelea kupoteza mali zao na wakati mwingine kunyanyasika zaidi kutokana na mila hiyo ya wanamke anapofiwa na mume kulazimishwa na ndugu upande wa mwanaume kurithiwa na mwanandugu ambae ameteuliwa na familia ya upande wa mume.
"Wajane wamekuwa wakipokonywa mahali mbali mbali zikiwemo nyumba , mashamba na vitu mbali mbali vya thamani ama wakati mwingine kufukuzwa kabisa na watoto iwapo ataonyesha kupingana na maamuzi ya wanafamilia hao ya kurithiwa "alisema Bi Mahenge
Kuwa kupitia kikundi cha cha waraghbishi wa jamii waliowezeshwa na TGNP wameanza kupita katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Mbeya vijijini na kutoa elimu kupitia matamasha mbali mbali kama njia ya kuelimisha jamii kuepuka mila hizo potofu.
Alisema hata kasi ya maambukizi ya VVU katika wilaya hiyo ya Mbeya vijijini na mkoa wa Mbeya kwa sehemu yamekuwa yakichangiwa na mila hizo za kurithi wajane.
Bi Mahenge mbali ya kuipongeza taasisi ya TGNP kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa jamii na kuijengea jamii uelewa kuhusu harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi katika muthadha wa mjadala wa madai ya wanawake katika uchaguzi mkuu 2015 hivi sasa wanawake ,watoto na wazee wameanza kufikiwa na elimu hiyo kiasi cha jamii kuanza kuachana na mambo kandamizi dhidi ya makundi hayo.
Katika hatua nyingine Bi Mahenge alisema kuwa mbali ya serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii sera yake kutaka wazee wenye miaka kuanzia miaka 60 kupatiwa huduma za bure za matibabu ila kwa kata hiyo bado wazee wameendelea kukosa huduma hiyo ya bure na badala yake wanapofika katika maeneo ya huduma za afya husumbuliwa zaidi ama kuandikiwa dawa za kwenda kununua.
Kwa upande wake afisa mawasiliano wa TGNP Bw Melkizedeck Karol alisema kuwa lengo la mtandao huu kutoa elimu kwa wanahabari ni kutaka kuendelea kutoa elimu kwa jamii na kwa pamoja kuweza kupaza sauti yenye kuleta mabadiliko kwa jamii dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Bw Karol alisema kuwa kwa mwaka huu TGNP inatoa mafunzo kama hayo kwa wanahabari kutoka kanda mbali mbali na kutaja maeneo ambayo mafunzo kama hayo yanaendelea kuwa ni pamoja na Kishapu, Tarime, Morogoro na Mbeya .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)