Pages

Wagombea urais Nigeria mchuano ni mkali

Masanduku ya kura nchini Nigeria
Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye madarakani, Goodluck Jonathan.
Lakini majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayajatangaza matokeo na mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali.
Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)