Pages

Usiku wa Mwanamke Duniani Machi 8


Gusa Gusa Band, Sabaha Muchacho, Afua Suleiman  na Shakila kutoa burudani

Na Mwandishi Wetu
Asia Idarous Khamsin (Fabak Fashions) inakuletea Usiku wa Mwanamke Duniani (Woman Celebration), utakaofanyika Jumapili ya Machi 8  ndani ya ukumbi wa Safari Carnival uliopo Mikocheni B, Jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Fabak Fashins, Asia Idarous Khamsin aliwaomba Wanawake kujitokeza kwa wingi usiku huo maalum kwani ni usiku wao na utakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo burudani ya taarab kutoka kwa bendi ya Gusa Gusa

huki waimbaji nguli wa taarab, Sabaha Muchacho,  Afua Suleiman  na Shakila wakitarajiwa kutoa burudani.
“ Karibuni wanawake wote ndani ya Safari Carniva, Kwa kiingilio cha sh 10,000/=. Ni  usiku wa Jumapili wa Machi 8, Nyoote munakaribishwa” alibainisha Asia Idarous Khamsin.

Asia Idarous Khamsin alisema vazi maalum la usiku huo ni ‘African print’, Ambapo pia kutakuwa na zuria jekundu ‘Red carpet’  kwa ajili ya picha za kumbukumbu litakalopambwa na wabunifu na wanamitindo mbalimbali usiku huo.

Aidha, usiku huo pia  Wanaume wanakaribishwa kujumuika pamoja na kufurahia pamoja.
Kwa upande wa Tikiketi zinapatikana Fabak fashions na Safari Carnival Mikocheni.
WAHI TIKET YAKO MAPEMAAA TUPIGIE 0713263363 or 0784263363.

Wadhamini wa usiku huo wa Mwanamke duniani ni pamoja na Fabak fashions, Mashughuli Blog, Vijimambo blog, Michuzi Media Group, Magic Fm, 8020fashion blog, Mo dewji  blog,Clouds fm, Eventlight na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)