Pages

Ujamaa watoa msaada katika kituo cha kulelea yatima



 Mwasisi na Mratibu Mkuu wa Kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network Bw. Lusekelo Mwandemange akikabidhi msaada kwa Bi. Zainab Bakary Maunga wa kituo cha kulelea  yatima cha Maunga Centre.
Bi. Mwajuma Njaritta  kutoka kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network akimkabidhi mmoja wa watoto Msaada wa vitabu kwa niaba ya watoto wengine katika kituo cha kulelea  yatima cha Maunga Centre.
 
 Baadhi ya Misaada iliyotolewa na kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network
 Mwanzilishi na Mkuu wa kituo cha kulelea  yatima cha Maunga kilichopo karibu na Kituo cha Polisi cha Hananasif  Kinondoni Bi. Zainab Bakari Maunga akitoa shukurani zake kwa kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network kwa kuleta misaada mbalimbali katika kituo hicho.
 
 Mwasisi na Mratibu Mkuu wa kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network Bw. Lusekelo Mwandemange akizungumza jambo wakati wa kutoa misaada hiyo na kuongeza kwamba huu ni mpango ambao wanaufanya kwa nchi nzima lengo ni kuwasaidia watu wasiojiweza, na pia ametoa ahadi ya kuendelea kutoa ushirikiano na kuendelea kusaidia zaidi kwa wale wasiojiweza. 
 
 Katibu Mkuu wa Kituo cha kulela yatima cha Maunga akitoa neno la Shukurani baada ya kupokea misaada hiyo na kuwasihi watu wengine waguswe ili waweze kusaidia kama hawa walivyofanya
 Mmoja wa watoto akitoa Shukurani zake kwa niaba ya watoto wenzake baada ya kupokea Msaada huo.
 Baadhi ya watoto wakiwa pamoja na wanakundi wa Kikundi cha Ujamaa Intellectuals Network 
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)