Pages

safari za KQ zarejeshwa

Marufuku juu ya safari za anga za shirika la ndege la KQ yafutwa .
Hatimaye marais Uhuru Kenyetta wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania wamekubaliana kufutilia mbali maagizo ya Mamlaka ya anga nchini Tanzania kupunguza idadi ya ndege za Kenya zinazotua nchini Tanzania na agizo la Wizara ya maliasili ya Kenya kupiga marufuku magari ya Tanzania kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Katika makubaliano hayo ndege za Kenya Airways sasa zitafanya safari zake kama kawaida nchini Tanzania na magari ya Tanzania yataruhusiwa kuchukua watalii na abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Kutoka Dar es Salaam Arnold Kayanda na taarifa ifuatayo.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernald Membe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya viongozi hao wakuu wa nchi hizo mbili kukutana nchini Namibia walikokwenda kuhudhuria maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia na kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo.
Awali kabla ya uamuzi wa marais hao, magari ya Tanzania yaliyokuwa yakichukua watalii katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, yalipigwa marufuku na serikali ya kenya katika agizo lililotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii Phyllis Kandie, ambapo baadae Tanzania nayo kupitia mamlaka ya Anga ya nchi hiyo ikaagiza ndege za shirika la ndege la Kenya, Kenya airways zinazoingia Tanzania kupunguza safari kutoka 42 kwa wiki hadi 14 pekee.
Makubaliano ya marais hao yanakuja siku chache baada ya mzungumzo ya mawaziri wa utalii wa Tanzania na Kenya kuvunjika mwishoni mwa wiki kufuatia pande hizo mbili kushindwa kufikia muafaka kuhusu magari ya Tanzania yaliyopigwa marufuku uwanja wa Jomo Kenyatta. Huku pia mamlaka ya anga ya Tanzania na ile ya Kenya nazo zikishindwa kufikia muafaka kuhusu kupunguza safari za ndege za kenya zinazoingia Tanzania.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)