Pages

Nyumba, magari mawili yateketezwa kwa moto katika vurugu eneo la Olasiti jijini Arusha leo

Nyumba hiyo ikiungua moto
Sehemu ya nyumba hiyo na gari 
Moja ya magari yaliyochomwa moto
Gari lingine lililochomwa moto
Majirani na wapita njia wakiangalia nje ya nyumba hiyo.
Picha na Gadiola Emmanul wa Tanzania Bloggers Network
Vurugu kubwa zinaripotiwa kutokea leo maeneo ya Olasiti jijini Arusha baaada ya habari ambazo bado kuthibitishwa rasmi zimeanza kufuatia mtu mmoja kukuta mfanyakazi wake wa kike akiwa  amelala  na anayedaiwa kuwa mpenzi wake ndani ya nyumba anayofanyia kazi. 
Inasemekana baba mwenye nyumba alikasirika sana kwa kitendo hicho na akampiga huyo kijan hadi akafa. Ndipo marafiki wa huyo anayedaiwa kuuwawa wakakusanyika nyumbani hapo na kuchoma moto nyumba na magari mawili kabla askari wa kutuliza ghasia kufika na kupambana nao kwa masaa kadhaa. Habari kamili na rasmi itawajia mara baada ya kupatikana

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)