Pages

News Alert:Zitto Kabwe ajiunga rasmi na chama cha ACT

Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe (pichani juu akisaini kitabu baada ya kupewa kadi) sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana  Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.

Hili limetokea  siku moja tu baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
 ACT-Tanzania: kirefu chake ni Chama cha Alliance for Change and Transparence Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)