Pages

News Alert:Watu 39 wahofiwa kupoteza maisha kutokana na mvua kubwa kunyesha Mkoani Shinyanga

Sehemu ya mabaki ya nyumba zilizobomolewa na mvua kubwa iliyonyesha katuika kijiji cha Mwakata, wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga na kusababisha vifo vya watu 39 na wengine 60 kujeruhiwa, usiku wa kuamkia leo Juatano Machi 4, 2015
 WATU 39 wamekufa, baada ya kuangukiwa na nyumba zao, kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, Jumanne usiku wa kuamkia leo Machi 4, 2015.
Akithibitisha taarifa hizo, kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema, maafa hayo yametokea katika kijiji cha Mwakata, kata ya Isaka, wilayani Kahama na kwamba watu wengine 60 wamejeruhiwa vibaya huku mifugo kadhaa, ikiwemo Ng'ombe, Mbuzi na kuku, navyo vimekumbwa na maafa. Huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka, kwani zoezi la uokoaji linaendelea licha ya changamoto ya kutokuwa na vifaa vya kutosha vya uokozi.




No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)