Pages

Maharamia waziteka meli mbili za Iran

Maharamia wa Somalia wateka nyara Meli mbili za Iran
Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia mihadarati na Uhalifu kimesema kuwa maharamia wameteka meli mbili za Iran za kuvua samaki katika ufuo wa Somalia.
Utakeji huo ni wa kwanza kufaulu tangu mwaka 2012.
Ushikaji doria na matumizi ya walinzi wenye silaha umesaidia kupunguza uharamia katika ufuo wa Somalia, ambao awali ulikuwa ukishirikisha zaidi ya meli 200 kwa mwaka.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wafanyakazi 48 wametekwa nyara katika uharamia huo.
Taarifa hiyo inasema kuwa meli hizo, zilizokuwa zikivua samaki bila kibali katika fuo hizo za Somalia zimepelekwa katika kijiji cha Pwani cha El Huur katikati mwa Somalia.
Ingawa uharamia ulikuwa umepunguka, idadi ya wavuvi haramu imeongezeka.
Uvuvi haramu ndio ulioanzisha mtindo wa kuteka meli Somalia.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa iwapo meli za kigeni zitaendelea kuvua samaki kimagendo katika ufuo wa Somalia, visa vya uharamia navyo vitaongezeka.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)