Pages

Kijiji cha Gongoni Wilaya ya Kilosa waadhimisha siku ya wanawake duniani

Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty alleviation in Tanzania  , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi, Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
 Mmoja wa Mashuhuda Juliana Bi. Salum ambaye amepata haki Miliki ya Ardhi akielezea Jinsi gani ambavyo itamsaidia katika Maendeleo yake na jamii kwa ujumla.
Mshereheshaji MC Chadieli G. Senzighe akiendelea kutoa Mwongozo katika Sherehe hizo.
 Elizabeth Luoga ambaye pia amepata Hati Miliki ya Ardhi akielezea Furaha yake na Ushuhuda wake kwa kuwashukuru OXFAM kwa jitihada kubwa walizo zifanya na wanazo zifanya ili wanawake wapate umiliki wa Ardhi amewashauri wanawake kuwa umiliki wa Ardhi unawezekana.

 Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Gongoni, Kilichopo Kata ya Rudewa 
Tarafa ya Kimamba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Bi. Grace Robertson 
Kanwakaita akitoa utambulisho kwa wageni mbalimbali ambao walifika katika Sherehe ya wanawake wakiwemo, Wakulima na wamama wafugaji walio katika eneo hilo,Opata,shirikisho la Ardhi,OXFAM, Mviwata,Ungo na wagani wengine waalikwa.
 Profesa Majourin Mbilinyi Mwanamke mwanaharakati, Katika Sherehe hizo alisema kwamba wanawake wengi hawana kipato katika kupata umiliki wa ardhi, Ameipongeza Serikali ya kijiji ya Gongoni kwa kuwapatia Haki miliki ya ardhi wanawake alisema kuwa ipo haja ya kubadili mfumo wa umiliki wa ardhi kwa sababu ardhi ipo lakini wamiliki ni wenyefedha na iliyobaki kiasi ndio wanagombania wafugaji na wakulima wadogo wadogo na kusababisha Migogoro. Mwisho alisema kuwa wanawake wanahaki sawa ya kumiliki ardhi.
 Mama Shujaa wa Chakula 2012 Anna Oloishuro , Akiongea wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani katika kijiji cha Gongoni , alisema katika kazi zake kama mama shujaa wa Chakula anapigania wanawake wapate umiliki wa Ardhi kwa kuwa Ardhi ni uhai, aliongeza kuwa wanawake wananyimwa haki ya kumiliki ardhi jambo ambalo sio sahihi hivyo ni jukukumu lake kupigania hilo, Mwisho aliwapongeza wote waliopata hati miliki za Ardhi.
 Marcelina Charles Kibena Mwanachama wa Shirikisho la ardhi Morogoro akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani , katika maoni yake alizungumza juu ya mgawanyiko wa Rasilimali na ardhi haupo sawa kabisa amesema kuwa ardhi kubwa inamilikiwa na mabepari na wenye fedha ambao aidha ni watanzania au watu waishio nje ya Tanzania ambao hao ndio wanaleta mgongano mkubwa katika kumiliki ardhi,Alisema watu wanazidi kuongezeka lakini ardhi haiongezeki ambapo pia hilo ni tatizo la kuleta migogolo ya Ardhi. Mwisho alisikitika kuona watoto hawasomi na wamejikita katika kilimo na Ufugaji alisisitiza watoto hao wanahaki ya kwenda shule na kuja saidia maendeleo ya kijiji na jamii kwa ujumla hapo baadae.
 

Eluka Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam  akiendelea kutoa mwongozo katika Sherehe hiyo
 Mratibu wa Mradi wa Haki za wanawake kumiliki Ardhi (WAOPATA) Joseph Pupa akielezea kwa ufupi maelezo ya Hati za Ardhi ambazo walipata wanawake mbalimbali pamoja na wanakijiji wengine wa Gongoni
 Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongea na wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ikiwa ni wiki ya maadhimisho hayo, alipongeza harakati za kuwawezesha wanawake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umiliki wa Ardhi, ambapo alisema kuwa OXFAM itahakikisha kila aliyeomba hati ya Kumiliki Ardhi ataipata, pia ameshukuru Taasisi zengine zisizo za kiserikali kuendelea kusaidiana ili kuleta maendeleo.


 
Meza Kuu wakifurahia Burudani 
 
Burudani ikiwa inaendelea 
 Baadhi ya wanakijiji wakipokea Hati Miliki za Ardhi
Wanakijiji wakipata vijarida
 Wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe hizo
Hata watoto walikuwa bize wakisoma Vipeperushi na Vijarida



No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)