Pages

Kambi ya kupima afya bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5

DSCN9331
DSCN9215
Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Kambi ya kupima afya bila malipo kwa watoto wadogo, itakayofanyika Jumapili ya Machi 8 mwaka huu. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy na kulia ni mwakilishi wa shule ya Kibugumu, Mwalimu Mzamili Ally.
Na Andrew Chale modewji blog
Imeelezwa kuwa, Sensa ya mwaka 2012 ilionesha kuwa asilimia 42 ya watoto chini ya miaka 5 hapa Nchini Wamedumaa, asilimia 16 wana uzito pungufu (wako underweight), asilimia 5 wamekonda (marasmic) wako kwenye kadi nyekundu ya mtoto.
Hayo yamesemwa jana Machi 4, jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa juu ya kambi ya upimaji wa afya kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 5, itakayofanyika Jumapili ya Machi 8, katika shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, wilaya ya Temeke.
Dk. Mzige alibainisha kuwa kama ilivyo kwa watu wazima, upimaji wa afya ya watoto wenye umri chini ya miaka 5 una manufaa makubwa kwa mtoto, familia na jamii ya watanzania wote.
Ambapo alibainisha kuwa, tatizo la utapia mlo kwa watoto hapa nchini imepelekea Tanzania kuwa nafasi ya tatu katika Bara la Afrika, Lishe duni kwa watoto na wajawazito huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ikiongoza na Ethiopia ikiwa ni ya pili kwa tatizo hilo la utapiamlo.
DSCN9217
Hata hivyo Dk. Mzige alibainisha kuwa, utapiamlo huo unaonekana nchini upo kwenye mikoa inayozalisha chakula na matunda kwa wingi ikiwemo ya Morogoro, Mbeya, Tanga, Rukwa, Iringa na Manyara.
Pia alieleza kuwa tatizo lingine ni la utapiamlo la kula chakula kupita kiasi kama vyakula vyenye wanga na sukari kwa wingi, mafuta kwa wingi na kuleta maradhi/magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watoto na watu wazima.
Aidha, Dk. Mzige alisema kuwa elimu sahihi dhidi ya kupambana na maradhi hayo ya utapiamlo, yatatolewa kwenye kambi hiyo huku akisisitiza wazazi kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani itakuwa ni ya kipekee na faida kwao na kwa watoto wao.
“Tujitokeze kupima afya zetu na pia watoto hasa wadogo. Hivyo kambi hii itakuwa msaada mkubwa kwani tutachunguza yale magonjwa mengi yanayowakabili watoto wengi hapa nchini.” Alisema Dk. Mzige.
DSCN9242
Dk. Mzige akionyesha mswaki wa mti ambai ni wa asili, ambapo alishahuri watanzania kuwa na tabia ya kubadilisha miswaki yao kila baada ya miezi mitatu, ama kutumia miswaki ya miti ambayo inasaidia kuboresha meno.
Akitoa baadhi ya takwimu zinazowakabili watoto wengi hapa nchini, ni pamoja na :
Watoto 130, walio chini ya umri wa miaka 5 hufa kila siku hapa Nchini kwa ajili ya utapiamlo (Malnutrition-Lishe duni).
Upungufu wa wekundu wa damu asilimia 59 kwa watoto wenye miezi 6 hadi 59. Asilimia 33 ya watoto chini ya miaka 6 wana ukosefu wa vitamin A.
BANGO SANGHO, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy alisema kuwa kwa kushirikiana na Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), ya Jijini Dar es Salaam ambapo wameandaa kambi hiyo ya kupima afya bila malipo kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ni faraja kwa jamii hiyo kwani watoto wengi hapa Nchini wamesahulika katika kupimwa afya zao.
DSCN9265
Dk. Mzige akionesha Yai ambapo alibainisha kuwa Yai sio zuri kwani lina Cholesterol hivyo mtu anashahuriwa kula mayai matatu kwa wiki hasa ya kuchemsha.
Amit Nandy aliwataka wananchi wa Kigamboni na maeneo mbalimbali kuwapeleka watoto wao katika shule ya Msingi, Kibugumu kwa ajili ya kupimwa afya zao hizo ikiwemo magonjwa yanayowakabili watoto wengi.
“wazazi wote tunawaomba kujitokeza kwa wingi, Machi 8, katika shule ya Msingi Kibugumu mukiwa na watoto wenu pamoja na makadi ya kliniki ilikuweza kupata huduma ya matibabu bure.
Madaktari bingwa na matabibu watapima magonjwa mbalimbali ikiwemo Afya ya kinywa, Uzito, Ukaguzi na ushauri wa lishe. Pia watakaobainika kuwa na matatizo maalum ya kiafya watapewa rufaa” alieleza Amit Nandy.
Ambapo alibainisha kuwa, huduma hizo za matibabu zinatarajiwa kutolewa kuanzia asubuhi ya saa tatu hadi saa saba mchana. (Saa 3:30 asubuhi-Saa 7-30 mchana).
DSCN9264
Dk Mzige akionyesha soseji ambapo alisema kuwa ulaji wa soseji sio mzuri kwa afya hivyo watu wanatakiwa kuepuka ama kupunguza.
DSCN9252
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)