Pages

Jihadi John bado kitendawili

Mohamed Emwazi maarufu Jihadi John
Waandishi wa BBC ndio wa kwanza kukutana na baba wa Mohammed Emwazi, maarufu kwa jina la Jihadi John ambae amekuwa akionekana katika kanda za video Islamic State akiwachinja mateka.
Jasem Emwazi amehojia na maafisa wa serikali ya Kuwait ambao wanajaribu kukusanya taarifa za mtoto wake. Mwandishi wetu, Mark Lowen, kutoka Kuwait amekutana na baba ya Mohamed Emwazi
Jasem Emwazi hakuonyesha hisia zozote pindi alipoingia ofisi ya wakili wake nchini Kuwait kukutana na waandishi wa BBC ambao ndio wa kwanza tangu mtoto wake alipojitambulisha kama mpiganaji katika picha za video za Islamic State.
Akiwa amevaa vazi jeupe, alininyooshea mkono. Nami nikasalimiana nae kwa lugha ya kiarabu na yeye akanijibu, lakini alitoka chumbani muda mfupi tu baada ya kukataa kufanyiwa mahojiano.
Wakili wake amesema bwana Emwazi yuko katika hali ya mshtuko na kuongeza kwamba amehojia na maafisa wa serikali ya Kuwait kwa muda wa zaidi masaa mawili na kuachiliwa bila jina lake kutajwa kwamba ni mshukiwa.
Mke wake na binti yake hawakuhojiwa, alituambia wakili huyo. Bwana Emwazi alirudi nchini Kuwait kutoka Uingereza mwaka jana mwezi wa Novemba, wakili wake amesema taarifa za vyombo vya habari kwamba amerudi hivi karibuni ni za kupotosha.
Ameongeza kusema kwamba bwana Emwazi hafanyi kazi hapa kama taarifa hizo zinavyodai. Alipoulizwa ni lini bwana Emwazi alizungumza na mwanae, au iwapo aliitambua sauti yake katika picha za video, wakili huyo alisema hatapenda kuzungumzia maswala binafsi.Crdt BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)