Pages

FA:Wenger akiri kupendelea kombe la mabingwa

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa amekuwa akichezesha kikosi hafifu katika michuano ya FA
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa amekuwa akichezesha kikosi hafifu katika michuano ya FA ilikuimarisha ushindani wa the Gunners katika kombe la mabingwa Ulaya
Habari inawadia wakati the Gunners wanajiandaa kukabiliana na Manchester United, kuwania taji la FA katika hatua ileile walioambulia kichapo cha 4-0 katika msimu wa mwaka wa 2008.
Mechi hiyo ilikuwa imekaribiana sana na mechi yao ya mchujo wa kombe la kuwania ubingwa wa barani ulaya dhidi ya AC Milan.
"Ni wazi iwapo ratiba ya mechi ya FA imewekwa karibu sana na mechi za kuwania ubingwa wa bara ulaya kama kocha ni wajibu wao kubaini ipi kati ya mechi hizo ni muhimu.'' alisema Wenger.
''kama unawachezaji wazuri unawapumzisha na badala yake kuwachezesha wengine katika mchuano wa FA.
Wenger alifanya mabadiliko katika kinyang'anyiro cha mwaka wa 2008 akiwapumzisha wachezaji wanne wa kutegemewa na licha ya kichapo hicho dhidi ya United walifaulu kufuzu kwa robo fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya baada ya kutoka sare tasa na timu hiyo ya Italia.
Tofauti na mwaka huo msimu huu vijana wa Wenger wanamlima wa kukwea baada ya kuambulia kichapo cha 3-1 mikononi mwa Monaco katika mkondo wa kwanza wa raundi ya kumi na sita bora uwanjani Emirati.
Hawatakuwa na mechi nyengine hadi tarehe 17 mwezi huu na hivyo huenda ikamruhusu Wenger ama Professa Wenger kuwachezesha nyota wake wa kutegemewa bila ya hofu ya kuwapoteza kwa majeraha.
Kocha wa Man united
Iwapo hali ni shwari Wenger huenda akawania ushindi wake wa kwanza uwanjani old Trafford tangu mwaka wa 2006.
Wenger anaamini kuwa matokeo ya mechi hiyo ya FA itaisaidia Arsenal kubaini kasi yake katika uwaniaji wa nafasi nne bora katika ligi kuu ya Premia.
Arsenal inaalama moja pekee mbele ya United ambayo inashikilia nafasi ya nne katika jedwali la ligi kuu ya Premia ya Uingereza.
Wenger "mechi ya jumatatu itakuwa mechi ya kukata na shoka maanake iwapo timu inashinda mechi kubwa na yenye hadhi kama hii wachezaji wake huwa wanaimarika kisaikolojia na motisha wao unawasaidia kushinda mechi zaidi''BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)