Pages

Elimu ya Jinsia lazima Uingereza

Wanafunzi wako hatarini kujiingiza kwenye vitendo vya Ngono bila kufahamu
Elimu ya Jinsia haijawahi kuwepo kila mahali katika jamii ya Waingereza.Lakini ipo kila mahali..kwenye Televisheni, matangazo na hata shuleni.Katika nchi ambayo Picha za ngono zimepigwa marufuku, zinaweza kupatikana kirahisi kwa njia ya Mtandao.
Viashiria vya uwepo wa vitendo vya ngono katika jamii ni mimba za utotoni.
Huku idadi ya wasichana wanaopata ujauzito ikiripotiwa kushuka , ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Uingereza bado iko nafasi ya nne kuwa na idadi kubwa ya Wasichana wajawazito katika nchi za jumuia ya Ulaya.
Hata hivyo jitihada zimeendelea kuonyeshwa na kuripotiwa kuzaa matunda katika kuhakikisha elimu ya Mahusiano na jinsia mashuleni inatolewa.
Serikali ya Uingereza inaona kuwa inahitaji kuongeza jitihada zaidi katika eneo hili.Waziri wa Elimu Nicky Morgan amesema Watoto wanakabiliwa na shinikizo kubwa katika maswala ya Ngono, hivyo wanahitaji msaada ili kuepuka hatari hii.
Serikali inataka kushughulikia kwa kuwapa vijana wadogo nyenzo za kuwezesha kuhimili vitendo vya mapenzi na watu wa rika lao ili kuepuka shinikizo la kimaumbile ambalo wanakutana nalo bila kujifahamu.
Taasisi ya kujitolea itakayoandika mitaala mipya ya kufundishia shuleni inasema maoni ya umma kuhusu udhalilishaji wa watoto nchini Uingereza yamedokeza umuhimu wa shule kufundisha wanafunzi kujiweka katika hali ya usalama wao na wenzao.
Wanaounga mkono elimu ya jinsia wanasema kwamba ushauri wa serikali kwa shule hautoi msisitizo wa kutosha na wanataka elimu ya jinsia na mahusiano yawe masomo ya lazima kwa wanafunzi wote.BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)