Pages

Chelsea yatoka sare na Southampton

Chelsea
Chelsea imeendeleza uongozi wake katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Southampton katika mechi ya msisimuko mkubwa iliochezwa katika uwanja wa darajani.
Diego Costa aliipatia Chelsea uongozi kupitia kichwa kizuri kabla ya Dusan Tasic kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya Nemanja Matic kumchezea visivyo Sadio Mane katika lango la Chelsea.
Kocha wa Chelsea Mourinho
Kipa wa Southampton Frazer Forster alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya Oscar,Eden Hazard na Loic Remy.
The blues sasa inaogoza ligi ikiwa na pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi wa ligi ya EPL Mancity waliocharazwa bao moja kwa nunge dhidi ya Burnley.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)