Pages

Baraka Shelukindo to tahadhari juu ya matapeli wa mitandao

unnamed (4)
Dear Friends
Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na tapeli mmoja ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook accounts kwa majina mbali mbali kama Justin Stan,James Brown,Onesmo,Felister Julius, Anthony Yohana au Yohana Anthony na mengineyo mengi.
Mtu huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika mtandao wa kijamii wa Facebook

Urafiki ukiwa umekamilika kwa maana ya friends request kutoka kwake and acceptance kutoka kwa victim amekuwa akiwaambia marafiki zake hawa wa Facebook kuwa yeye ni muajiriwa sehemu mbali mbali tofauti katika kila account hizi za facebook kama kwa mfano kwingine akidai anafanya Vodacom Mlimani City, kwingine akidai anafanya Tanesco Makao Makuu,PPF na sehemu nyingine kadhaa na amekuwa akiwaahidi kwamba ana watu wenye uwezo wa kuwaunganishia kazi sehemu hizo kwa sharti la wanaotaka kazi kujikusanya na kufikia idadi ya watu watano na wakilipa kiasi cha shilingi 50,000 kila mmoja basi watapata nafasi za kazi hizo.

Wakati mwingine amekuwa akiwa wadanganya baadhi ya watu kuwa yupo mkoani kikazi au akihudhuria semina na kwamba mdogo wake anashida ya dharura ya pesa kama shilingi 25,000 au 30,000 na kuomba marafiki wamtumie na kuwaahidi atawarudishia mara atakapokua free, amekuwa akitoa namba mbali mbali za simu mojawapo zikiwa hizi 0785412653 na 0688081032. Wale walioshtuka amekuwa akiwatukana matusi makubwa ya nguoni bila uoga.

Natoa tahadhari kwa watu wote kujihadhari na kufanya urafiki na watu msio wajua, kuzingatia umakini haswa katika mambo ya pesa, pia kujua watu wa namna hii ni wengi sana online haswa kwenye social media. Nashauri uki suspect mtu wa design hii basi wasiliana na polisi na ikibidi kumtengenezea mtego wa kumnasa.

Vijana tunatakiwa tuchape kazi kwa nguvu na sio kutafuta njia za mikato. Hakuna hadithi yeyote niliyowahi kuisikia ya aliyefanikiwa katika maisha kwa njia ya mkato. Mwana fundi ni kusoma kwa bidii ili elimu yako ikupatie ajira.

Mwisho naomba marafiki zangu wooote mnisaidie kurepost message hii kwani naamini itawaokoa wengi (vulnerable) ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa hawajui utapeli huu wa online.

Picha hiyo hapo juu ni yangu na ndio amekuwa akiitumia kwenye account nyingi za facebook.

Mimi ninaamini Mungu na hivyo huyu bwana Siku zake 40 zipo karibu. Napenda pia kwa namna ya kipekee nawashukuru wale wote (zaidi ya 10) waliotumia muda wao kunitafuta na kunipa taarifa hizi muhimu walipomshtukia Tapeli huyu.

Mwenyezi Mungu awabariki saana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)