Pages

Balozi wa Marekani nchini Korea ya Kusini ashambuliwa kwa kisu

Muonekano wa Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini, Mark Lippert baada ya kuchomwa kisu
Mark Lippert (katikati) akiwa anajifuta damu.
Kim Ki-jong akiwa amekamatwa na polisi baada ya kumchoma kisu balozi wa Marekani.
Mark Lippert akisaidiwa kunyanyuka baada ya kuchomwa kisu.
BALOZI wa Marekani nchini Korea Kusini, Mark Lippert ameshambuliwa kwa kisu usoni na katika kifundo cha mkono wake leo na mshambuliaji aliyekuwa anapinga mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani.
Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zaman, Mark Lippert, akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.
Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayahatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa katika  shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi. Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote.
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kama hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung  amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)