Pages

Akina mama wa kikundi cha Citizen Foundation watoa msaada

Akina mama Wa Citizen Foundation wakiongozwa na askari polisi wa kituo cha  chang'ombe wakati wakifanya maandamano kutoka kituoni hapo kwenda  kukabidhi msaada wa magodoro hospitali ya temeke.
 Akina mama wa Citizen Foundation wakiwa nje ya Hospitali ya Wilaya ya Temeke na walikokwenda kukabidhi magodoro.
 Mwenyekiti wa Citezen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi moja ya magodoro, Amosi Kabelege ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Hospitali ya Temeke.
 Mwenyekiti wa Citizen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi maji ya kunywa, Bi. Ashura aliyelazwa hospitalini hapo.
Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Amani Malima alimshukuru Mwenyeti wa Citezen Foundation kwa masaada wa magodoro waliotoa hospitalini kwake jana.

Akina mama wa Kikundi cha Citizen cha Tabata jijini Dar es Salaam, jana kilitoa magodoro 50 na katoni 25 za maji na 25 za soda aina ya Cocacola ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Akina mama Duniani.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Lilian Wasira alisema wameguswa sana na tatizo la akina mama kujifungulia sakafuni ndiyo maana wakaona watoe msaada huo.

Lilian alisema, wameamua kufanya hivyo badala ya kusherehea siku hiyo kwenye kumbi za burudani huku wenzao wakijifungulia sakafuni.

Mwenyekiti huyo alisema hawataishia Temeke tu bali wanatarajia kufanya harambee nchi nzima kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha huduma ya afya inaboreshwa.

Magodoro hayo yana thamani shilingi milioni 2,740,000

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)