Pages

Ajali ya ndege:rubani alifungiwa nje

Ndege ya Germanwings ilipokuwa ikisafiri katika anga la Duesseldorf nchini Germany mwaka 2014.
Ndege ya shirika la Germanwings, Airbus yenye namba A320 na namba ya safari 4U 9525 iliyokuwa  ikitoka Barcelona nchini Hispania kwenda Duesseldorf nchini Ujerumani ilianguka kutoka angani mpaka chini ya aridhi kwa muda wa dakika 8 umbali wa futi 38,000 katika milima ya Alps iliyopo nchini Ufaransa.
Mkurugenzi wa shirika la ndege la Germanwings, Thomas Winkelmann amesema wasafiri 72 kati ya 144 walikuwa raia wa Ujerumani. Wahanga wengine walikuwa ni wanafunzi 16. Wakati huo nchi ya Hispania ikisema watu 51 walikuwa ni raia wa nchini humo. Katibu wa UK Foreign, Philip Hammond amehakikisha kuwa watu 3 walikuwa ni Waingereza.
wengine walikuwa ni kutoka nchi za Australia, Argentina, Iran, Venezuela, Marekani, Uholanzi, Colombia, Mexico, Japan, Denmark na Israel.
Ramani ikionesha eneo la ajali ya ndege ya Ujerumani
Uchunguzi wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyo alikuwa amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka.
Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa ameondoka kufanya nini lakini sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka ufunguliwe mlango.
Milima ya Alps, eneo ambalo ajali ya ndege ilitokea.
Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la New York Times.
Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema kwa kinywa wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.
''Hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali hiyo ''
''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati majuzi tu wala haikuwa na hitilafu yeyote''.
Ajali ya ya ndege ya Germanwings ilivyotokea.
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.
Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo .
Wanafunzi katika shule ya Haltern-am-See nchini Ujerumani wakilia baada ya wenzao kupata ajali kwenye ndege ya Germanwing.
Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.
David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea.
Waokoaji wakijadiliana katika eneo la ajali ya ndege hiyo.
Pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu, na hatua walizochukua kunusuru janga hilo.
Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege?
Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini walichokiacha na mambo kama hayo.
Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa isiyoeleweka. 'Niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa, bado hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana'.
Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo, bado hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa, kuhusika katika ajali mbaya kiasi kile.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)