Pages

Adebayor arejea uwanjani

Nimerejea sasa adai Adebayor
Mshambulizi wa Tottenham Hotspurs raiya wa Togo Emmanuel Adebayor, amesema kuwa matatizo yaliyokuwa yanamsumbua yamekwisha.
Mshambulizi huyo wa Tottenham mwenye umri wa miaka 31 alirejea uwanjani mwishoni mwa wiki baada ya zaidi ya miezi miwili akipasha moto benchi .
Adebayor sasa amesema kuwa anafanya kila jitihada ilikurejelea hali yake ya awali alipokuwa akicheka na wavu na kuwatesa walinzi wa safu za upinzani.
Nyota huyo wa Togo alishuhudia timu yake ikiambulia kichapo cha mabao 3-0 mikononi mwa Manchester United.
''Kwa hakika mambo mengi tu yamefanyika maishani mwangu mambo ambayo yameniathiri kwa kiasi kikubwa lakini sasa hali imerejea kuwa shwari namshukuru mola''
Adebayor,amefunga mabao 2 katika mechi 16
''Sote ni binadamu ,leo utafaulu kufanya jambo kesho itakuwa zamu ya mwengine lakini msimu huo maisha yalinipiga chenga, na nikayaruhusu kuingilia mchezo wangu na umakini wangu''
'' sasa nimerejea uwanjani mzima,mzima.''
''sasa mimi si kijana barubaru mwenye umri wa miaka 21 la hasha ,mimi sasa nimegonga miaka 31 na hivyo napaswa kuonesha ukomavu wangu uwanjani''
Adebayor aliwakera wengi White Hart Lane baada ya kupoteza makali yake mbele ya lango mapema katika msimu huu ambapo aliwahi kuifungia klabu yake mabao mawili pekee katika mechi 16 alizocheza.
Hali hiyo butu imempelekea bwana huyo kusalia kama mchezaji wa akiba huku mshambulizi mtajika Harry Kane akizidi kupata umaarufu na mashabiki na imani ya kocha.
Emmanuel Adebayor, amesema kuwa matatizo yaliyokuwa yanamsumbua yamekwisha.
Mwisho wa mwezi Desemba Adebayor nusura ahamie West Ham united lakini mkataba huo ukatiba siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.
hakuna anayejua hadi leo nini kilisababisha kufeli kwa mkataba huo.
Adebayor hata hivyo hajawahi sema iwapo ananuia kuendelea kuichezea Tottenham hata baada ya mwisho wa msimu huu.
''Tumesalia na mechi 9 na hilo linamaanisha nitakuwa hapa kwa zaidi ya miezi miwili, chochote chaweza kutokea.Alisema mchezaji huyo
Mashabiki wa White Hart Lane walimzoma wakimlaumu kwa kuwa butu na kusababisha ushindani wa timu hiyo kudorora.bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)