Pages

Upandikishaji wa Kichwa kwa Mwanadamu katika Mwili mwingine sasa unawezekana

Upandikishaji wa kichwa cha binaadamu hadi katika mwili mwengine sasa unawezekana kulingana na wanasayansi
Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa.
Madaktari watazindua mradi huo katika kongamano wakati wa msimu wa joto ,kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017.
Mtu atakayeongoza mpango huo ni daktari raia wa Italy Sergio Canavero kutoka kundi moja la wanasayansi mjini Turin.
Anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani.
Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa ,kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi.
Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya.
Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)