Pages

Ngumi kupigwa Tandika Maguruwe Feb 22 Mwaka huu

Bondia Imani Daudi Mapambano kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika club ya Super D iliyopo Shile ya Uhuru Dar es salaam Mapambano anajiandaa na mpambano wake na Mohamed Kibwana utakaofanyika Feb 22 katika ukumbi wa Musoma bar uliopo Tandika Maguruwe 
Bondia Imani Daudi Mapambano kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika club ya Super D iliyopo Shile ya Uhuru Dar es salaam Mapambano anajiandaa na mpambano wake na Mohamed Kibwana utakaofanyika Feb 22 katika ukumbi wa Musoma bar uliopo Tandika Maguruwe 
 IMANI DAUD MAPAMBANO AKIWA NA IBRAHI,U CLASS KING CLASS MAWE
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumu za chembe na kidevu bondia Imani Daud Mapambano anaejiandaa kuzidunda na Mohamed Kibwana mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Tandika Maguruwe Feb 22 
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akipambana na Imani Daud
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akipambana na Imani Daud
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi za kurufuka kwa kunyoosha mkono  bondia Imani Daud Mapambano anaejiandaa kuzidunda na Mohamed Kibwana mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Tandika Maguruwe Feb 22 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

Bondia Imani Daud Mapambano amendelea kujifaa katika club ya Super D iliyopo Kariakoo shule ya Uhuru Dar es salaam kabla ya kukabiliana na bondia Mohamed Kibwana siku ya Feb 22 katika ukumbi wa Musoma Bar uluopo Tandika Maguruwe Dar es salaam

akizungumzia mandalizi ya mpambano wake  Daud amejinasibu kwa kusema kuwa siku hiyo ato kuwa na msaliamtume kwa kuwa yupo fiti zaidi na ana uchu wa kucheza mchezo mzuri kwa kuwa ndio kwanza kaenda kujiandaa katika GYM mpya hivyo atopenda kuwangusha
mchezo huo wa raundi nane utakaosimamiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO chini ya Rais wake Yassin Abdallah 'Ostadhi' amesema mabondia hawo watapima uzito siku ya jumamosi na kucheza siku ya jumapili katika ukumbi wa musoma bar uliopo Tanduka Maguruwe
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)